Magazetini: CDU/FDP wanunua data Posta,Uislamu Ujerumani
3 Aprili 2018
Tukianza na gazeti la Der neue Tag la mjini Weiden kuhusu kuuzwa kwa data za wateja na shirika la posta kwa vyama vya CDU na FDP, mhariri anaandika.
"Ni kitu gani shirika la posta linafahamu kuhusu sisi na kuuza kwa mtu mwingine taarifa hizo kwa fedha. Data kuhusu uwezo wa kununua, matumizi ya benki, jinsia, umri, elimu, mahali anakoishi, iwapo ana familia na iwapo anamiliki gari. Posta iliuza data hizi za raia kama ilivyofanya kwa idara ya serikali inayohusika na magari na ofisi ya ardhi. Vyama vilifaidika na hilo? anauliza mhariri. Wanaweza kutumia data hizo kwa ajili ya kuwafikia watu hao kwa njia ya matangazo."
Gazeti la Stuttgarter nachrichten akizungumzia suala hilo la kuuzwa kwa data za wateja anaandika:
"Posta imekuwa kama buibui katika mtandao wa data nchini Ujerumani. Kila mtu nchini Ujerumani ana anuani yake , na inatumbukia moja kwa moja katika benki yake ya data, na kama unataka data hizo ni lazima uombe kwa maandishi. Hii ina maana gani, inamfanya mtu apate kizungumzu. Shirika tanzu la Posta - Deutsch Post Direkt GmbH lina kiasi ya taarifa za binafsi za watu zaidi ya milioni 34 katika majumba yapatayo milioni 24 nchi nzima. Hii anaandika mhariri inaweza kuifanya kashfa ya kuvuja kwa data za watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Facebook kuona wivu. Hii inaonekana kuwa haina madhara na ni halali kisheria lakini inaonekana kivingine."
Kuhusiana na mjadala kuhusu Uislamu nchini Ujerumani gazeti la Rhein-Zeitung la mjini Koblenz linaandika.
Kile kinachokera kuhusiana na mjadala huu juu ya Uislamu ni kwamba hauna mwelekeo wowote na mara kadhaa ni kutokana na matamshi tu ya kijinga. Kwasababu mwanasiasa kama Horst Seehofer alikuwa anataka kusema nini kwa matamshi yake kwamba "Hakuna uhusiano kati ya Uislamu na Ujerumani" Kwamba Uislamu haupaswi tena kuwapo nchini Ujerumani ? Kwamba Uislamu haupaswi kufundishwa hapa Ujerumani ? Misikiti ifungwe? Waislamu wote wanapaswa waondolewe ? Mtu anaweza kuzungumzia hilo kwa maneno mengine. Hosrt Seehofer na chama chake cha CSU wanahatarisha amani ya Ujerumani, inasababisha ugumu wa Waislamu kujumuika katika jamii ya Ujerumani, na kuongeza hali ya usalama na hatari zaidi
Gazeti la Frankfuerter Rundschau , kuhusiana na hali ya mapambano kati ya Wapalestina na Israel linaandika.
"Katika ripoti ya Umoja wa Mataifa tayari ilishatolewa tahadhari, kwamba kuna hatari Gaza katika mwaka 2020 itakuwa sehemu ambayo haiwezekana mtu kuishi. mapambano yaliyotokea katika siku ya Ijumaa kuu , wakati Wapalestina karibu 30,000 walifanya maandamano yaliyopewa jina la maandamano ya kurejea walijikusanya katika uzio wa mpaka na Israel , na suala hilo kuliweka katika hali ya kuangaziwa kimataifa. Miito kwa pande zote , kujizuwia haisaidii tena. Mradi mahsusi ya ujenzi wa bandari, mifereje ya maji taka inayofanyakazi, uwezekano wa kuwekwa nishati ya jua kwa ajili ya umeme haya yanaweza kupunguza kwa njia halisi msuguano huo. Mzingiro mkali wa eneo hilo ni lazima ufike mwisho, ili watu wa Gaza wasipoteze kabisa matumaini."
Mwandishi: Sekione Kitojo / inlandspresse
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman