Watu 11 wanaripotiwa kupoteza maisha nchini Rwanda kutokana na maambukizo ya virusi vya Marburg, ambayo hadi sasa yameshawakumba watu 29 tangu vilipobainika kwa mara ya kwanza mnamo tarehe 27 Septemba. Amina Abubakar amezungumza na mwandishi wa habari anayeishi mjini Kigali, Khalid Hassan, kuhusiana na kusambaa kwa maradhi hayo.