Mfumko wa bei Ulaya umevuka kilele chake, hakuna mdororo
14 Februari 2023Mfumuko wa bei unatarajiwa kupungua kasi lakini ukibakia juu, na hasa kwa mataifa yalioko nje ya kanda inayotumia sarafu ya euro.
Makadirio hayo yanakuja wakati bei ya gesi asilia inaendelea kushuka kutoka viwango vya kihistoria vya katikati hadi mwishoni mwa mwaka 2022.
Soma pia:Umoja wa Ulaya waahidi kusimama na Ukraine bila kuchoka
Tume hiyo pia imekadiria kwamba uchumi wa kanda hiyo utaepuka kunywea katika robo ya sasa ya Januari hadi Machi, na hivyo kuzuwia mdororo wa kiufundi.
Hali hii inafuatia ukuaji wa asilimia 0.1 katika robo iliyopita. Lakini halmashaurki kuu ya Ulaya pia imeonya kwamba watumiaji wataendelea kuhisi shida ya kupungua kwa uwezo wa kununua, kwa kuwa mfumuko wa bei unabakia juu ya asilimia 5.
Makadirio ya ukuaji wa muda mrefu kwa mwaka 2024 hayajabadilika, yakisalia kwa asilimia 1.6 kwa Umoja wa Ulaya, na asilimia 1.5 kwa kanda ya sarafu ya euro.