Malalamiko ya chama cha majaji DRC
20 Novemba 2024Siku nne baada ya kukamilishwa kwa vikao kuhusu sheria nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, chama cha kitaifa cha majaji kilikuwa na mkutano mkuu mjini Kinshasa jana jioni ambapo kilitangaza nia yake ya kuwasilisha malalamiko yao kwa viongozi wa ngazi za juu serikalini na pia watafikisha malalamiko yao mahakamani.
Ni mwenyekiti wa chama cha majaji nchini Congo mwendesha mashtaka Edmond Issofa aliyeyasema hayo kwa wanahabari, baada ya mkutano wao mkuu.
Soma pia: M23 waukamata tena mji wa Kalembe mashariki ya Kongo
Miongoni mwa masuala yanayopingwa na majaji, kati ya mapendekezo mia tatu na hamsini na tisa yaliotangazwa ilikuiponya sheria nchini Congo inayotajwa kukabiliwa na hali mbaya, ni mapendekezo kama kubadilisha baraza kuu la majaji, nakuwa baraza kuu la sheria, ambamo majaji watakuwa wanashiriki pamoja na rais na pia waziri wa sheria.
"Tunajiandaa pia kukutana na wanachama wa baraza kuu la mahakimu ilikulifafanua hilo. Tunazo ripoti zilizosainiwa na wale walioongoza warsha na pia tunazo sauti pamoja na video za kikao. Hiyo ni kwa upande wa mbinu za utetezi na mbali na mbinu za utetezi, tutawakilisha mashtaka yetu mbele ya sheria kwani mliona kwamba umati wote ulikubali hili na nyakati zinazofuata, tutakwenda kwenye korti," amesema Edmond Issofa.
Na ili kutaka kujua ikiwa mbinu watakazozitumia majaji ilikurekebisha makosa yaliyofanywa na mhariri wa ripoti ya vikao kuhusu hali ya jumla ya sheria nchini DRC, zitafua dafu, nilizungumza na mwanasheria Frank Lutahwa, mchambuzi wa masuala ya sheria na pia mwalimu wa sheria kwenye vyuo mbalimbali vya Beni.
"Huwezikuwa mshtaki na kuwa jaji kwa wakati mmoja. Ikiwa mahakimu watawakilisha mashtaka yao kwenye mahakama, watayawakilisha kwa mwendesha mashtaka mkuu wa jamhuri. Hapo kuna kasheshe kwani hawezikuifanyia kazi mashtaka hayo kwani naye ni mhusika kwenye mahakama."
Mapendekezo mia tatu na hamsini na tisa yaliyotangazwa wikendi iliyopita, baada ya kukamilishwa kwa vikao kuhusu hali ya jumla ya sheria nchini Congo, miongoni mwake mwake yakiwemo yale yaliyo na nia ya kuyarekebisha matatizo yanayotibu magonjwa yanayotajwa kuikabili sekta ya sheria nchini hapa.
Soma pia: Makubaliano ya kusitisha mapigano DRC yavunjika
Na majaji wakiwa ndio wanashukiwa kuwa chanzo cha matatizo yote yanayotwikwa vyombo vya sheria, mwenyekiti wa chama cha kitaifa cha kitaifa cha majaji wa Congo Edmond Issofa anasema, kwamba wanaosababisha shida katika sekta ya sheria nchini humu ni wengi.
"Wafanyakazi kwenye sekta ya sheria ni kiungo kya sheria, waziri wa sheria naye ni kiungo kya sheria, wadau wengine nao ni viungo, mawakili nao ni viungo. Yaani wanaposhuku sheria kwamba inaugua, ni utandawazi huo."
Pendekezo la kubadilisha baraza kuu la majaji na kulifanya kuwa baraza kuu la sheria, linapingwa na majaji wote wa nchi hii, wanaosema kwamba uwepo wa rais pamoja na waziri wa sheria kwenye baraza tarajiwa la sheria, kutasababisha utawala wa sheria kupoteza uhuru wake.