SiasaSudan
vita Khartoum kitisho kwa mpango wa kusitishwa mapigano
20 Aprili 2023Matangazo
Makabiliano hayo yanatishia kuvuruga juhudi za karibuni za mpango wa kusitishwa mapigano wakati serikali za kigeni zikitafuta mbinu za kuwahamisha raia wao waliokwama katika mzozo huo.
Mpango wa kuweka chini silaha kwa saa 24, ambao ulianza kutekelezwa jana jioni, ndio jaribio kubwa kabisa mpaka sasa la kusitisha mapigano hayo kati ya jeshi na vikosi vya wanamgambo wa Rapid Support Forces - RSF. Kiasi ya watu 330 wameuawa na 3,300 kujeruhiwa katika mapigano hayo tangu yalipoanza Jumamosi, kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani - WHO lakini idadi huenda ikawa kubwa kwa sababu miili zaidi inapatikana mitaani. Juhudi za kidiplomasia zinaendelea kujaribu kuyarefusha makubaliano ya kusitishwa mapigano.