Mapigano ya Sudan yashika makali kusini mwa Khartoum
26 Agosti 2023Mapigano nchini Sudan yameendelea jana Ijumaa wakati Umoja wa Mataifa ukitoa onyo kali kuhusu athari za vita hivyo na kusema kuwa vinatishia kuiteketeza nchi hiyo.
Wanamgambo wa RSF walianzisha mashambulizi mapya kwenye kambi muhimu kusini mwa mji mkuu, eneo ambalo jeshi na vikosi vya wanamgambo vimekuwa vikipambana kuchukua udhibiti tangu Jumapili.
Vita kati ya mkuu wa kijeshi Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo, ambaye ni kamanda wa jeshi la RSF, vimepamba moto tangu Aprili mosi. Vita hivyo vimeenea kutoka mji wa Khartoum na eneo la magharibi la Darfur hadi jimbo la Kordofan na Jazira, na kuua maelfu na kuwalazimisha mamilioni kukimbia makazi yao.
Burhan ajitokeza hadharani miezi 4 tangu vita vianze
Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa zaidi ya watu milioni 4.6 wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mapigano hayo.