Marekani yasema yafuatilia kwa karibu kinachoendelea China
29 Novemba 2022Waandamanaji pia wanadai uhuru zaidi wa kisiasa.Ikulu ya Marekani imesema rais Biden anafuatilia kinachoendelea China katika wakati ambapo pia ndani ya Marekani yamezuka maandamano ya kuonesha mshikamano na waandamanaji nchini China.
Msemaji wa baraza la usalama la Marekani John Kirby amewaambia waandishi habari jana Jumatatu kwamba wanatazama kinachojitokeza kutoka China lakini rais Biden hatozungumza kwa niaba ya waandamanaji duniani isipokuwa waandamanaji watajipazia sauti wenyewe.
soma zaidi: China: Maandamano yaenea kupinga sera kali za kudhibiti UVIKO
Ingawa ametilia mkazo kwamba Marekani inaunga mkono haki ya waandamanaji.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani jana ilisema sera ya China kuhusu kuzuia virusi vya Corona imepindukia mipaka na kwamba itakuwa vigumu kwa nchi hiyo kudhibiti usambaaji virusi hivyo kwa kutumia mkakati wake huo.
Chanzo: afp