Marekani yazishutumu China na Urusi kuilinda Pyongyang
26 Agosti 2023Marekani imezishutumu China na Urusi kwa kuzuia tamko la pamoja la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ufyatuaji wa makombora ya Korea Kaskazini, likiwemo jaribio la wiki hii la urushaji wa satelaiti ya kijasusi angani.
Wakati wa mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama, wanachama 13 kati ya 15, wote isipokuwa Moscow na Beijing walilaani jaribio la pili la kijasusi la Pyongyang katika muda wa miezi mitatu.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield alisema hilo linapaswa kuwa suala linalo waunganisha lakini tangu mwanzoni mwa 2022, Baraza hilo limeshindwa kutekeleza ahadi zake kwa sababu ya China na Urusi.
Aidha pia ameshutumu kitendo cha maafisa wa Urusi na China kuhudhuria gwaride la kijeshi la Korea Kaskazini mwezi uliopita.